Picha na Yohana Ndone
NJOMBE
Na Nimrod Mgoye.
Serikali ya kijiji cha idundilanga katika Wilayani Njombe Mkoani Njombe ikumbukwe kwamba miezi kadhaa iliyo pita ilitoa tamko kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la njia panda ya
magereza waondoke na kuelekea katika soko mpya lililopo katika mtaa wa joshoni.
Tamko hilo la Serikali lilitolewa kutokana na soko hilo kuwa mahali ambapo sio
salama kwa wafanyabiashara hao kwa kuwa lipo jilani na barabara mbili kati ya barabara ya kuelekea songea na
barabara ya kuelekea magereza.
Katika hatua nyingine wafanyabiashara hao wameendelea kuonekana wakifanya biashara
katika soko hilo lililo kuwa limezuiliwa kipindi hicho huku wengine walipo ulizwa na waandishi wa habari walisema kuwa kule waliko kuwa wamepelekwa kulikuwa kunawaingizia hasara ukilinganisha na pale walipo sasa.
wakaiendelea kuzungumza na chombo chetu cha habari wamesema kuwa kuludi kwao kwenye soko hilo nikutoka na kuto kuwepo kwa wanunuzi wa mahitaji hayo kwa uwepo wa soko lile kuwa mbali.
hali kadhalika Chombo chetu cha habari kiliendelea kuongea na wafanyabiashara wa eneo hilo huku wengine wakigoma kutoa ushirikiano huku mmoja wapo akisema kuwa yeye hawezi kuongelea suala hilo hali ambayo inaonesha
wanafanya biashara kimakosa katika eneo hilo.
waandishi wa habari katika jitihada za kumtafuta msemaji wa mtaa wa kijiji hicho ili kuzungumzia suala hjilo la kuludi katika soko hilo ziligonga mwamba.
katika ofisi yake ya mtaa alikutwa mwanafunzi wa mafunzo ya vitendo na akaonyesha ushirikiano kwa kusema kuwa mtendeji wa eneo hilo yupo katika ziara ya kikazi ambapo eneo alilo kuwepo hakulitaja.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking