Serikali ya Burundi inasema matangazo ya mashirika ya utangazaji ya BBC na VOA yamepigwa marufuku nchini humo kwa miezi sita kuanzia Mei 7
mwaka huu kwa, 'kutofuata sheria zinazotoa muongozo wa uandishi habari nchini' na 'kukiuka maadili ya kikazi'.
Inaishutumu BBC kwa kushindwa kumwajibisha mwanaharakati wa Burundi katika mahojiano aliyofanyiwa katika idhaa ya kifaransa ya shirika hilo.
Hatahivyo waandishi wa habari wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida nchini humo.
Matangazo ya BBC hupeperusha nchini Burundi kupitia masafa ya FM na kwa kupitia radio mbili washirika.
BBC inajitahidi kuwasiliana na serikali ya Burundi kuhusu uamuzi huo.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking