picha ya mtandaoni.
NJOMBE
Na yohana ndone
wakazi wa wilaya ya njombe mkoani humu wailalamikia mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kwa utoaji wa bili kubwa ukilinganisha na matumizi yao ya kila siku.
wakizungumza hayo jana baada ya kukutana na waandishi wa habari walipo tembelea kwenye ofisi za ulipaji wa bili hizo katika ofisi za idara hiyo katika hatua nyingine wakazi hao wakaweka bayana kuwa bili za matumizi yao ya kila siku zimekuwa nikubwa kila mwezi na mwezi mwingi huwa ni ndogo.
msemaji wa maji mkoani humu ambaye ni kaimu mkurugenzi wa ofisi hiyo DOGRAS MKWAMA amekanusha malalamiko hayo kwa kusema kuwa idara yake ipo makini kwa usomaji wa mita na ufungaji wa gharama kamili kwa wateja wao.
pia kaimu huyo akaongeza kwa kusema kuwa wanachi wengi hawana elimu ya kutosha juu ya usomwaji wa mita zao na akasema kuwa inapaswa sasa kuwapa elimu ili kutoa malalamiko hayo.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking