Njombe
Na
chrispin kalinga.
Kanisa
la Romani Kathoriki Wilayani Njombe Mkoani
Njombe leo katika ibada ya Misa ya pili iliyo ongozwa na Askofu wa kanisa hilo baba Askofu
ALFRED MALUMA ambayo ililenga haswa
kuazimisha siku ya sikukukuu ya kupaa kwa Bwana Yesu Kristo ambapo amefundisha mambo mengi haswa kuwa heshimu wakina
mama.
Akiyazungumza
hayo Kanisani mbele ya wahumini kuwa watu wote wanatakiwa kuishi maisha
matakatifu kipindi hiki cha nyakati za uzima huku akiwataka kumkumbuka bikira
maria ambaye pia ndiye mama yake
Yesu.
Yesu.
Askofu
huyo amewapa kauli mbiu isemayo ‘Mama Maria huku wengine wakihitikia kwa
kusema wetu sote’.
Sambamba
na hayo kiongozi huyo amesema kuwa wote watubu Dhambi zao na kumfuata Bwana Yesu ili siku ya hukumu ikifika wawe wamekombolewa na akaongeza kwa
kuwataka waumini wote kuwaheshimu wazazi wote haswa wakina mama.
Katika
hatua nyingine Askofu huyo akawapokea wanachama wapya wa chama cha wawata {WWT}
ambacho chama hicho ni chama cha umoja wa kinamama wa kathoriki Tanzania na
akawapongeza kwa kujiunga katika chama hicho akawasihi wazidi kuomba mungu huku
na kuwaombea wengine.
Kwa
upande wao wakinamama wa kanisa hili wamezungumza na waandishi wa habari kuwa
siku hii ya sikukukuu ya kupaa kwa Bwana Yesu kwa upande wao wameipokea vizuri
kwa kumwomba mungu katika sara na pia wamebarikiwa kwa sikukukuu ya kuadhimisha
miaka 150 ya kanisa kathoriki tangu lianzishwe kwake.
Pia Askofu akamaliza kwa kusema kuwa wote waishi maisha ya kumwomba Mungu na wazidi
kuombiana kwa mungu ili kifanikisha safari ya kuelekea Mbinguni.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking