Sondag, Mei 06, 2018

RAIS MAGUFULI ATEMA CHECHE KWA VIONGOZI


Rais Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa serikali kuacha kutoza ushuru kwa wananchi wanaosafirisha bidhaa na mazao ambayo hayajafika uzito wa tani moja,  kwakuwa bunge mwaka 2017 lilipitisha sheria ya kufuta tozo zaidi ya 87 katika sekta ya kilimo.

Rais Magufuli alisema hayo jana Mei 05, 2018, katika sherehe za uzinduzi wa daraja Magufuli lililopo katika mto Kilombero mkoani Morogoro, na kusema kuwa jukumu la serikali ya awamu ya tano ni kutatua kero za wananchi hasa wakulima na kama Rais wa nchi anazijua kero hizo kwasababu amekua kiongozi wa serikali kwa zaidi ya miaka 20.

“Nataka nitoe wito kwa viongozi, ukimuona mtu amebeba magunia 10 ya mpunga maana yake hayajafika tani moja, mpishe wala usimuangalie mwache asafirisha mizigo yake, nataka viongozi wenzangu mnielewe nilizunguka Tanzania nzima kuomba kura kwa ajili ya kuwatetea wananchi, ninafahamu kero za wananchi, wewe kama ni mtoza ushuru nenda ukalime ukajitoze ushuru mwenyewe” alisema Rais Magufuli.

Rais Dkt. Magufuli ameongeza kuwa serikali haiwezi kuwa kikwazo cha maendeleo kwa wananchi na kuongeza kuwa anataka daraja hilo liwanufaishe wananchi wa Morogoro na kuwasihi wakulima kusafirisha bidhaa chini ya tani moja kama wanataka kuepuka kutozwa ushuru.

Daraja la Magufuli lipo katika mto Kilombero, barabara kuu ya Kidatu Ifakara  na lina urefu wa mita 384,  limegharimu shilingi bilioni 61.2 kwa fedha za ndani.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking