Picha na Francis Malekela Baadhi ya wanafunzi walio fanya Ziara ziwa Nyasa.
MBEYA .
NA MWANDISHI WETU
Wanachuo wa Chuo cha Uandishi wa Habari Eckros School of Journalism kilicho Mkoani Njombe wamefanya Ziara ya kimasomo katika Kijiji cha
Matema Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwenye
Ziwa Nyasa kwa lengo la kujifunza kwa vitendo.
Wanafunzi hao
wamezungumza na wakazi wanao zungukwa na ziwa hilo kwa kujifunza vitu vingi haswa historia ya ziwa hilo kuanza kwake
na hadi mahali lilipo sasa.
Moja ya
mwanachuo wa Chuo hicho anaye soma fani ya Uandishi wa Habari Daniel Lameck
Tumbo amesema kuwa Ziara hiyo ya Matema amejifunza mambo mengi haswa kuanzishwa
kwa Ziwa hilo kuwa lilijulikana tangu zamani zilizo kadiliwa.
Aidha kijana huyo akaongeza kwa kusema kuwa ziwa nyasa
lilitoka na bonde la ufa na akaongeza kusema kuwa ziwa hilo lina samaki aina mbalimbali lakini pia samaki wenye
rangi mbalimbali waliopo kwenye ziwa hilo.
Wanafunzi
hao wameongozana na Mkuu waChuo hicho pamoja na walimu wa Chuo hicho huku mkuu
wa chuo hicho Erick Mlelwa akizungumza na chombo chetu cha habari cha Mubashara blog kwa kusema kuwa lengo la
kuwapeleka wanachuo hao kufanya ziaraMkoani humo ni kuwafundisha kwa vitendo kwa
lengo la kujibia mtihani yao ya mwisho .
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking