MBEYA- MATEMA
NA CHRISPIN KALINGA
Wakazi wa Kijiji cha Matema Wilayani Kyela Mkoani
Mbeya wamezungumza na waandishi wa habari juu ya uwepo wa Ziwa Nyasa na wananufaika vipi kwa uwepo wa ziwa hilo na
huku wengine wakisema kuwa licha ya mafanikio hapakosi changamoto.Moja ya mvuvi wa ziwa hilo anaye fahamika kwa jina
la Kyando amewaambia waandishi wa habari kuwa ziwa hilo linafaida kubwa sana
kwa vijana wa maeneo hayo kwa kuwapatia fedha zakujikimu kila siku kwa uvuvi wa
samaki ziwani humo.
Akaongeza kwa kusema kuwa ziwa hilo limekuwa na
faida kubwa kwao na hata kwa Mkoa huo na nchi kwa ujumla kwa kujipatia watalii
kutoka maeneo ya nchi za jilani na baadhi ya wakinamama wa maeneo hayo wamesema
kuwa ziwa hilo kwa upande wao limekuwa na faida kubwa kwa kufanya biashara ndogondogo haswa migahawa na wakaongeza
kwa kusema kuwa mwambao mwa ziwa hilo wanatengeza vyungu kwenye maeneo hayo
kwaajili ya biashara.
Sambamba na hayo wavuvi wakamaliza kwakuimba
serikaka kuwasaidia vifaa vya uvuvi na huku wengine wakiomba wadhamini wanaoweza
kujitokeza kuwapa mitaji baadhi ya vijana ili wanunu nyavu za kuvulia samama
kwa viwango stahiki.Hali kadhalika ziwa nyasa matema limezungukwa na
wafanya biashara ambao huuza vinywaji na wengine kutengeneza baadhi ya maeneo
hayo kwa kuyaweka vizuri kwaajili ya watalii wanao watembelea.
Msemaji wa ziwa hilo Bwana kyando akasema kuwa
anapenda kuwakalibisha watu kutoka maeneo mbambali kwa kuja kutalii na kujione
vitu vingi ndani ya ziwa hilo haswa samaki aina mbalimbali zenye rangi .
Pia Elasto
Cassian kiongozi wa ziwa hilo aliye fumba kitengo chake ameongeza kwa kusema kuwa licha ya samaki hao
kuna jiwe ndani ya eneo la ziwa
linalo julikana kwa jina la PALIKYALA ‘Pana Mungu’ na akaongeza
kwa kusema kuwa kuna eneo ambalo limejitenga alimaaalufu kama pango ambalo
linaulefu kutoka kwenye ziwa hilo hadi makete mkoani njombe na akaweka wazi
kuwa pango hilo zamani lilikuwa linatumika kwaajili ya dua mbalimbali ikiwepo
kuomba mvua na kadhalika.
mubashara blog
+255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking