Na Maiko Luoga Ludewa
Mtoto Anaekadiliwa Kuwa na Umri wa Miaka Miwili Mwenye Jinsi ya Kiume Amekutwa Akiwa amefariki kando ya Mto Mhangachi Katika Uwanja wa Mpira wa Shule ya Sekondari Chief Kidulile Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe.
Kwa Mujibu wa maelezo ya Mashuhuda waliojitokeza katika Tukio hilo wamesema kuwa Mwili wa Mtoto huyo ulionekana Tangu Asubuhi ya Leo Mei 24 mwaka huu 2018 Wakati Wanafunzi Wa Shule ya Sekondari Chief Kidulile wakifyeka Nyasi katika Eneo la Kuzunguka Uwanja wa Mpira ndipo walipouona Mwili wa Mtoto huyo Ukiwa Umeanza Kuharibika na Kutoa Harufu kali.
Mashuhuda hao wamesema kuwa Marehemu amekutwa akiwa hana Kichwa na Kushindwa Kutambuliwa Kuwa Ni Mtoto wa nani na mwili wake Umebaki kuanzia katika eneo la Shingo, Kushuka hadi Miguuni ambapo Kichwa Chake Kinaonesha Kuwa Kimebondwa na Kuchakazwa Vibaya na Kusababisha Watu washindwe Kuitambua Sura ya Marehemu.
Muda Mfupi Baadae baada ya Kupokea Taarifa Kutoka kwa Wasamalia wema wakiwemo Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Sekondari Chief Kidulile Askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ludewa walifika Katika Eneo la Tukio na Kujionea Hali halisi ya Tukio hilo Ambapo Kaimu Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ludewa ASP Malimi N Malimi Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio hilo na Kusema Kuwa Chanzo cha Tukio hilo Bado hakijafahamika Maramoja na Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi Sambamba na Kuiomba jamii ya Ludewa Kutoa Ushirikiano katika Kubaini Muhusika wa Tukio hilo.
ASP Malimi Amesema Kutokana na Marehemu kutotambuliwa na Mwili wake Kuharibika kwasasa Jeshi la Polisi wilaya ya Ludewa linaendelea na Taratibu za Kisheria ikiwemo kupata Kibali ili Mwili wa Marehemu uzikwe kuanzia Kesho na endapo Ndugu wa Marehemu watajitokeza Taratibu nyingine zitaendele.
Kwaupande wake Daktari Frank Mwambasanga aliyeupokea na Kuufanyia Uchunguzi Mwili wa Marehemu katika Hospital ya Wilaya ya Ludewa Amesema Kuwa Marehemu alikuwa Jinsi ya Kiume anakadiriwa kuwa na Umri wa Miaka miwili na Kuongeza Kuwa Tukio hilo Linakisiwa kutokea Siku tano zilizopita ambapo Sababu huenda ikawa ni Ajali kwakuwa Mwili wa Marehemu umekutwa ukiwa na Majeraha, ambapo Baada ya Ajali hiyo Kutokea Huenda Mhusika wa Tukio hilo akaamua Kuutelekeza Mwili wa mtoto huyo.
Aidha Daktari Mwambasanga Baada ya Kuulizwa na Mwandishi wetu Kuwa Inawezekanaje ikawa Ajali na Kusiwepo taarifa zozote kutoka kwa jamii za Kupotea kwa Marehemu, Daktari Mwambasanga Alisema Kuwa Mtoto huyo pia huenda alikuwa anatokea Nje ya Mji wa Ludewa kwakuwa Baada ya Tukio hilo Kutokea Hakuna Mtu yeyote Ludewa aliyetangaza Au Kutoa Taarifa Kuwa Amepotelewa na Mtoto.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking