Mkurugenzi
wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis
Taletale maarufu Babu Tale, leo Mei 23, 2018 saa 6 mchana amefikishwa
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza kesi inayomkabili, akiwa
chini ya ulinzi wa polisi.
Babu
Tale, ambaye pia ni meneja wa mwanamuziki maarufu wa 'Bongo Fleva'
Diamond Platnumz, alikamatwa kufuatia amri iliyotolewa Februari 16, 2018
na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda Maalum, Wilbard Mashauri
iliyoelekeza kukamatwa mtuhumiwa huyo na ndugu yake, Idd Taletale.
Amri
hiyo pia, ilielekeza watakapokamatwa wapelekwe Gereza la Ukonga wakiwa
wafungwa wa kesi ya madai, hadi hapo mahakama hiyo itakapotoa maelekezo
mengine.
Hata
hivyo, Babu Tale hakuweza kupatikana na ndipo mahakama hiyo ikatoa amri
nyingine kama hiyo Aprili 4 mwaka huu. Tangu hapo wamekuwa wakitafutwa
bila mafanikio hadi jana alipokamatwa.
Mahakama
hiyo iliwaamuru kumlipa Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim
Mbonde kiasi cha Sh250 milioni, baada ya kupatikana na makosa ya
ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila
ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.
Leo
baada ya kufika mahakamani mbele ya Naibu Msajili, Ruth Massam, amewapa
muda wa dakika 10 pande zote wajadiliane namna ya kulimaliza suala
hilo.
Baada ya majadiliano hayo pande zote zilirudisha majibu kwamba hazikufikia maelewano yoyote. Hivyo Naibu Msajili, Ruth Massam alichukua uamuzi wa kuiahirisha tena kesi hiyo na Babu Tale kurudishwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Katika
kesi ya msingi, Sheikh Mbonde alikuwa akidai kuwa aliingia mkataba na
kampuni ya kina Babu Tale (Tiptop Connection) ili wamrekodi mahubiri
yake kisha wayauze na kugawana mapato.
Hata
hivyo baada ya kurekodi masomo saba, walimkatia mawasiliano na
alipowatafuta na kukutana nao wakamweleza kuwa wameamua kuachana na
mpango huo.
Sheikh
Mbonde alidai kuwa akiwa kwenye mahubiri Dodoma ndipo akakutana na
mikanda ya video katika mfumo wa DVD yenye mahubiri yake huku kukiwa na
namba za simu za viongozi hao wa Tiptop.
Sheikh
Mbonde alidai baada ya kufanya uchunguzi alibaini kuwa DVD hizo
zilikuwa zikiuzwa katika mikoa mbalimbali, ndipo akawafungulia kesi ya
madai ya fidia kutokana ukiukwaji wa Sheria ya Hakimiliki na
Hakishiriki.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking