Sondag, Mei 13, 2018

Tanzania yatinga nusu fainali Kombe la Dunia


Timu ya wasichana walio kwenye mazingira magumu ya Tanzania, imetinga hatua ya nusu fainali ya fainali za Kombe la Dunia kwa watoto waishio kwenye mazingira magumu nchini Urusi baada ya kuifunga Marekani kwa mabao 5-0.

Makanisa yavamiwa na kulipuliwa kwa mabomu


Watu waliojitoa mhanga wamevamia makanisa matatu nchini Indonsia na kuyalipua kwa mabomu, Milipuko hiyo imetokea katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Surabaya na kusababisha vifo vya watu 9, huku idadi hiyo ikitazamiwa kuongezeka.

Wizara Ya Afya Yamwaga Ajira 8,000 Sekta Ya Afya Nchini

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata kibali cha Ajira kwa sekta ya afya nchini cha kuwaajiri wataalam wa kada mbalimbali za Afya wapatao 8,000.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, (TMA) Yatoa Tahadhari ya Mvua Kubwa

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, (TMA) imetoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo ya Ukanda wa Pwani kwani mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha kuanzia leo.

Zari: Nilimpenda Sana Diamond Ila Alizidisha Dharau Nikaamua Kumtema

Aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amesema alimpenda sana muimbaji huyo na kila mtu alifahamu hilo ila dharau zilizidi, ndipo akaamua kuvunja mahusiano yao.

Aliyetaka Kumuhonga Zari Range Rova Apigwa Kibuti

Zari The Boss Lady amesema hamfahamu Ringtone Apoko ambaye ni msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya aliyetangaza kumnunulia mrembo huyo gari aina ya Range Rover Sport ya mwaka 2017.

ASKOFU WA ROMANI KATHORIKI NJOMBE ANENA MAZITO

Image result for bishop alfred maluma

Njombe

Na chrispin kalinga.

Kanisa la Romani Kathoriki Wilayani Njombe Mkoani Njombe leo katika ibada ya Misa ya pili  iliyo ongozwa na Askofu wa kanisa hilo baba Askofu ALFRED MALUMA ambayo ililenga haswa kuazimisha siku ya sikukukuu ya kupaa kwa Bwana Yesu Kristo ambapo amefundisha mambo mengi haswa kuwa heshimu wakina mama.

Waziri wa Afya: Upimaji UKIMWI baa sio lazima

Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema upimaji wa Kifua Kikuu (TB) na Ukimwi kwenye baa hautakuwa wa lazima.

Magazete ya Leo ya 13


Vrydag, Mei 11, 2018

Wanahabari Wamkalia Kooni Rais Kenyatta


KAMATI ya kutetea wanahabari nchini Kenya, imemuomba Rais Uhuru Kenyatta asiusaini muswada wa sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2017 uliopitishwa na Bunge la nchi hiyo hivi karibuni.

Mbosso Atoa Siri ya Video Zake


Muimbaji Mbosso kutoka label ya WCB, Mbosso amesema video za ngoma zake ambazo zinatoka kwa sasa zilifanyika kipindi kirefu sana.

Uwoya Ahama Nyumba Kuhofia Mzuka Wa Masogange

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amesema tangu rafiki yake Agnes Gerald ‘Masogange’ atangulie mbele ya haki amekuwa akihofia kutokewa na mzuka wake.

Mkurugenzi CDA Afikishwa Mahakamani Kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dodoma, jana ilimpandisha kizimbani aliyekuwa Mkurugenzi wa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Paschal Muragili kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka.