Donderdag, Junie 02, 2022

HABARI KUBWA KATIKA JARIDA LA LUDEWALEO JUNI 02, 2022

Habari kubwa katika Jarida letu la leo ni jengo la Ofisi kubwa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Ludewa linalo jengwa katika Halmashauri hiyo huku ujenzi wake ukiendelea kwa kasi ukilinganisha na kipindi kilicho pita kwa sababu ya mvua kubwa zilizo kuwa zikiendelea kunyesha.

Kukamilika kwa jengo hilo litatatua kero ya ukosefu wa Ofisi za idara mbalimbali zilizotawanyika.

Lakini pia Ukamilikaji wa jengo hilo litakuwa ni jengo zuri ambalo litawavutia watu wengi kuja kulitembelea kutokana na uzuri wa jengo lenyewe na wengi watatamani kupiga picha katika eneo hilo.

Aidha katika jarida letu la leo habari kubwa iliyo gusa mioyo ya watu wengi ni kutoka pale Kata ya Luana ambapo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg.Sunday Deogratias aliwaahidi wananchi wa Kata ya Luana  alipo kuwa akiwahutubia katika mkutano wa wawazi na kusema kuwa, Kata ya Luana ni miongoni mwa kata zinazo fanya vizuri haswa katika ukelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasà, Ujenzi wa vituo vya afya nk.

Hivyo kwa uunga mkono jitihada za wananchi wa Kata hii sasa nikiwa Kama Mkurugenzi nitatoa Bati 176 ambazo Mhe. Diwani Wilbard Mwinuka ameniomba.

Hivyo nawaombeni wananchi tuendelee kuiunga mkono serikali yetu kwa kuendelea kufanya kazi ili tutekeleze miradi yote inayo endelea kwenye kata hii "alisema Sunday Deogratias Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Ludewa" kauli hiyo aliitoa Mei 29, 2022.

Licha ya Miradi mingi inayo tekelezwa kwenye Wilaya ya ludewa, Diwani wa Kata ya Ludende  Mhe. Vasco Mgimba akishirikiana na wananchi wa Kata hiyo wamefanikiwa kuinua jengo la Mama na mtoto la kituo cha Afya cha  Ludende ambao Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ilitia mkono wake kuunga mkono juhudi za wananchi, lakini pia Diwani wa Kata hiyo bado amenyenyekea chini ya serikali kuomba kuungwa mkono ili kukamilisha jengo hilo ambapo awali serikali ilitupia mkono wake katika hengo hilo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Ludewa bado amewapa Imani kubwa wananchi wa Kata hiyo kwa kusema kuwa,

Serikali inatambua mchango mkubwa wa wananchi wa Kata hiyo ndio maana Walipo omba Halmashauri isaidie kwa awamu ya kwanza ilitekeleza na kwasasa Mhe. Diwani kaomba tena na sisi Kama Halmashauri tutaaungana na wananchi kukamilisha jengo hilo kwa Bajeti ya Mwaka 2022/2023.

Katika hatua nyingine katika jarida letu la leo Juni 02, 2022 Sehemu ya juu inaelezea Ujenzi wa chuo cha Ufundi VETA kinacho jengwa Kata ya Lugarawa pale shaulimoyo, ujenzi wake unaendelea na kwasasa upo kwa asilimia 20% ambapo ukamilikaji wake ni  mwishoni mwa mwaka huu, na kusuasua kwa mradi huo ni kutokana na mvua kubwa zilizo nyesha kwa kipindi cha mwezi January hadi Aprili.

Pia neema nyingine yamwagika tangu kuumbwa kwa ulimwengi barabara ya kutoka Mbwila hadi Lifuma inaendelea na uchimbwaji ambapo kukamilika kwa barabara hiyo itakuwa imeokoa gharama kubwa za usafiri ukilinganisha na wakati huu wananchi hulazimika kusafiri kwa kutumia Ziwanyasa (Mitumbwi na Boti)

Jitihada za Mhe. mbunge wa Ludewa  Joseph Kamonga zinaendelea kuzaa matunda, na ikumbukwe kwamba Jana Mei moja aliweza kuhoji Bungeni mambo mbalimbali ikiwemo uendelezwaji wa nguvu

za wananchi wake.


 

Dinsdag, Mei 17, 2022



Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Waziri Waziri Kindamba jana Mei 12, 2022 alitembelea kiwanda cha muwekezaji mkubwa wa Parachichi Mjini Makambako katika mkoa wa Njombe kinachojulikana kwa jina la AvoAfrica.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa pamoja na mambo mengine alikagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na muwekezaji wa kiwanda hicho haswa katika utaratibu mzima wa uchakataji wa Parachichi hadi hatua ya mwisho.

Katika hatua nyingine Mhe. Waziri Kindamba wakati akizungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi wa maeneo hayo alisema kuwa;

Ndugu wananchi wa Mkoa wa Njombe na Watanzania wote, nitumie nafasi hii kuwahakikishia wawekezaji wote kuwa, Njombe ni sehemu salama ya uwekezaji na tunawakaribisha wawekezaji wote kuja kuwekeza katika Mkoa wa Njombe katika sekta ya Viwanda, Kilimo, Uvuvi, Utalii bila kusahau Madini kule Ludewa_ ,*

Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Waziri Kindamba aliongeza kwa kusema kuwa;

Muwekezaji yeyote atakayekuja kuweka Mtaji wake Njombe tupo tayari kuwalinda kwa wivu mkubwa ili vijana wetu waendelee kupata Ajira.

Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Mkoa alisema kuwa Wawekezaji wanapokuja kuwekeza Njombe Serikali inapata faida kwa ulipwaji wa Kodi kutoka kwa wawekezaji hao lakini pia Wananchi wananufaika na mambo mbalimbali ikiwemo Ajira, mzunguko wa Biashara n.k.

Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

 

Umuhimu wa kipekee wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na:-

  1. Kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;

  2. Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;

  3. Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;

  4. Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;

  5. Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na

  6. Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.


Saterdag, Desember 14, 2019

CHUO TOKA NJOMBE CHAWANASUA VIJANA KWENYE JANGA LA ELIMU YA JUU NAFASI ZA MASOMO HIZI HAPA USIHANGAIKE KUANZIA DARASA LA SABA NAKUENDELEA MNAPOKELEWA

Kama utahitaji ufafanuzi zaidi piga simu au tuma ujumbe mfupi wa maadishi 0753121916 au  0620669137 utapewa ufafanuzi zaidi.

Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Eckros Njombe Tanzania.
Hapa ni wanafunzi wakiwa na mkurugenzi wa chuo pamoja na walimu.

Vrydag, November 22, 2019

Mambo yatakayokuepusha na ugonjwa wa kisukari



Ugonjwa wa kisukari ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza, ambayo husababishwa baada ya kongosho kushindwa kutengeneza 'insulin' ya kutosha ndani ya mwili.

Hukumu Ya Rais wa zamani wa TFF Jamal Malinzi na wenzake Kusomwa Disemba 5 Mwaka Huu



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itatoa hukumu dhidi ya Rais wa zamani wa TFF Jamal Malinzi na wenzake watatu December 05 mwaka huu.

Malinzi, Mwesigwa, Mwanga na Flora wanakabiliwa mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha Dola za Kimarekani 173,335.

Waziri wa Viwanda na Biashara Afanya Uteuzi wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).




mubashara blog +255753121916

Woensdag, November 20, 2019

Tatizo la Kutokwa na usaha Wakati wa Kukojoa

Tatizo la Kutokwa na usaha Wakati wa Kukojoa
KWA WALE AMBAO WATAHITAJI KUKUTANA  LAKINI PIA USHAURI NA MAMBO MENGINE WASILIANA NAMI  DOCTAR MWAKALINGA WASILIANA NAMI 0753121916 KWA MASHART NAAFUU.
 wa kuandika makala hii ya tatizo la kutokwa usaha wakati wa kukojoa umetokana na swali la msomaji wetu ambaye aliuliza hivi kwenye tovuti hii na hapa na mnukuu,
 " Dr MWAKALINGA  samahani sana mi nasumbuliwa nikikojoa mwisho wa mkojo unatoka kama usaha na sina dalili ya kaswende ambazo umezizungumzia nakuomba unisaidie’’.

UKIMWI BADO UPO !!!


Image result for ukimwi



Tohara kwa wanaume ni oparesheni inayohusu kuondolewa kwa sehemu ya ngozi au ngozi yote inayofunika kichwa cha uume, na imekuwa ikifanywa na baadhi ya watu katika makabila na dini mbalimbali kwa zaidi ya maelfu ya miaka.
Kwa sasa tohara kwa wanaume imeamsha mvuto mkubwa wa kisayansi na uchunguzi kwa sababu utafiti umethibitisha kuwa wanaume waliotahiriwa wana viwango vidogo vya maambukizo ya virusi vya ukimwi (VVU) kuliko wasiotahiriwa.

DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA HIZI HAPA

Sababu na dalili za Kuharibika kwa Mimba - Sehemu ya Kwanza
KWA WALE AMBAO WATAHITAJI KUKUTANA  LAKINI PIA USHAURI NA MAMBO MENGINE WASILIANA NAMI  DOCTAR MWAKALINGA WASILIANA NAMI 0753121916 KWA MASHART NAAFUU.
Kuharibika kwa Mimba ni nini?
Utangulizi
Kuharibu/kuharibika kwa mimba kwa njia ya kutoa kiinitete (embryo) au mjusi (fetus) kabla ya kutimiza umri wa kuweza kuishi nje ya mfuko wa kizazi hujulikana kama abortion 1. Mimba inapoharibika yenyewe kabla ya kutimia umri wa wiki 20 hujulikana kama miscarriage.

NJIA YA KUPATA MTOTO WA KIUME HII HAPA


KWA WALE AMBAO WATAHITAJI KUKUTANA  LAKINI PIA USHAURI NA MAMBO MENGINE WASILIANA NAMI  DOCTAR MWAKALINGA WASILIANA NAMI 0753121916 KWA MASHART NAAFUU.

Uzazi wa mpango una mambo mengi sana.. sio kuzuia mimba tu ndio uzazi wa mpango ila hata kupanga idadi na jinsia za watoto ni moja ya njia za uzazi

Mwezi wa tano ya mimba huwa alama ya kuwa umefikisha nusu ya ujauzito kwa wanawake wengi ulimwenguni




KWA WALE AMBAO WATAHITAJI KUKUTANA  LAKINI PIA USHAURI NA MAMBO MENGINE WASILIANA NAMI  DOCTAR MWAKALINGA WASILIANA NAMI 0753121916 KWA MASHART NAAFUU.” 
Mzazi hakati tamaa”.
Ukijitazama kwa wakati huu, umeanza kuonyesha mimba zaidi. kuna wanawake wengi walioanza kufanya  ununuzi wa nguo mpya kwa ajili nguo zao zimeanza kuwa ndogo. Ni vizuri kununua nguo ambazo zina uhuru wa kutembea na kuinama au unapolala.

Dalili za mimba ya miezi miwili NA ukuaji wake





KWA WALE AMBAO WATAHITAJI KUKUTANA  LAKINI PIA USHAURI NA MAMBO MENGINE WASILIANA NAMI  DOCTAR MWAKALINGA WASILIANA NAMI 0753121916 KWA MASHART NAAFUU.
Hongera!
Umefikisha miezi miwili ya mimba. Sasa hebu tujadiliane  zaidi juu ya maendeleo mwilini mwako na ule wa mwanako katika mwezi huu.
Ukiwa na mimba ya miezi miwili, unaweza kuwa na mchangamko na hisia mbali mbali, wakati mwingine, unaweza kuhisi  wasiwasi au kutoamini u mja mzito. Kwa wanawake wengi, Hizi ni hisia za kawaida na ni mabadiliko makubwa katika familia kuweza kupata mwana.