Vrydag, Junie 03, 2022

Habari kubwa katika Jarida la Ludewa ni pamoja na Jeshi la Polisi Ludewa laendelea kutoa elimu ya unyanyasaji wa kijinsia na Wananchi





Katika Jarida letu la leo ukiondoa habari  kuu yagazeti letu Leo nimekusogezea taarifa mbalimbali kutoka ndani ya Wilaya yetu.

Na moja ya habari hizo ni pamoja na Jeshi la Polisi Wilaya Ludewa linaendelea kupaza sauti kwa kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa kuwapa elimu ya Ukatili wa kijinsia na kuwasihi watanzania wote wa Wilaya ya Ludewa kuachana na vitendo vya kikatili ambavyo hivyo hupelekea vifo.

Aidha Inspector Violeth GIdeon amepaza sauti kwa kuzifikia Tarafa zaidi 3 za Wilaya ya Ludewa kwa kuendelea kuelimisha na Kuhamasisha kutokomeza Ukatili wa kijinsia huku akibainisha kwa kuwapa uhuru wananchi wote kutoa taarifa za ukatiki wanapo ziona katika kituo chochote cha Polisi.

Wananchi hupata fursa ya kuuliza maswali na kupatiwa ufumbuzi na huku Inspector huyo akiwasihi wanawake kuacha Ukatili kwa watoto na kwawaume zao na akawasihi wanaume kutoa taarifa katika Dawati la jinsia pindi wanapo fanyiwa ukatili na wanawake zao.

*"Nitumie nafasi hii hadhimu kuwasihi wanaume,msione haya kuja kutoa taarifa ya Ukatili pindi mkeo anapo kukatili nenda kituo cha Polisi Dawati la jinsia litakusikiliza na kutafuta suluhisho la tatizo hilo nakuwafanya muishi kwa Amani na Upendo."* alisema inspector

Pamoja na hayo mengi bado katika Jarida letu limetoa taarifa ya elimu ya lishe,ambapo hapo tunakumbushwa kuwa mlo bora kwa watoto wetu itasaidia kuondokana na Udumavu ambao kwasasa kwa Halmashauri yetu ya Ludewa  tunataka kuutokomeza kabisa Udumavu.

Katika hatua nyingine hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias alitangaza ajira 8 na mwisho wa kutuma barua za maombi ya kazi ni tarehe 08/06/2022 hivyo watanzania wote mnakumbushwa kutumia fursa hii kwa siku zilizo salia kuomba kazi.

Hali kadhalika wananchi wa Kata ya Milo Wilayani Ludewa wametoa hisia zao kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuziinua kaya masikini kwa Kuziwezesha fedha ambayo imewafanya maisha yao yabadilike.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mapogoro katani Milo wamesema TASAF imewawezesha na kufikisha kujiinua kiuchumi hukubwengi wao fedha hiyo wakiielekeza kwenye Mashamba na wengine wamenunua mifugo na kuifuga na kukarabati nyumba zao.

Lakini pia Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias ametuma salamu za pongezi kwa Kata ya Madilu kwa kuonesha ukomovu na shauku kubwa ya maendeleo ya Wilaya haswa katika eneo la elimu kwa kufanikiwa kujenga nyumba ya mwalimu wa shule ya msingi Madilu ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika mwaka huu.

Habari kubwa katika Jarida letu la leo Juni 03, 2022

 

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere anaendelea kuwaasa baadhi ya watu watakao dhubutu kukwamisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Kauli hiyo anaitoa kila mahala anapo endelea na ziara yake ya Kuhamasisha na kuelimisha watanzania wote waliopo ndani ya Wilaya ya Ludewa huku akiwaeleza umuhimu wa Sensa ya kwa maendeleo ya taifa letu.

Aidha Mhe. Andrea Tsere alisesema "zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka huu ni muhimu kwenye taifa letu, kwani kila mmoja wetu akihesabiwa serikali itajua namna ya kuhudumia wananchi wake haswa wakati wa kuandaa bajeti ukilinganisha na idadi ya Watu wake"

Kwa kuto hesabiwa mmoja utaifanya serikali ipate takwimu tofauti hivyo watu wangu kwanu wananchi wote tarehe 23/08/2022 kila mmoja anawajibu wa Kuhesabiwa asiwepo hata mmoja wa kukwepa jambo muhimu la kitaifa.


Donderdag, Junie 02, 2022

DC LUDEWA ATEMA NYONGO



Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere  ametoa onyo kwa mtu yeyote atakayeonekana kuvuruga zoezi la Sensa ya watu na makazi na kuahidi kumchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria ya nchi ikiwemo kulipia faini kiasi cha fedha kisichopungua Ml.1, Jela miezi sita au vyote kwa pamoja.

Kauli hiyo ameitoa katika mikutano ya kutoa elimu juu ya zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi iliyofanyika katika kata ya Luilo, Luhuhu pamoja na kata ya Manda.

Kwa mujibu wa Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo Isaac Ayengo amesema adhabu hizo zipo kwa mujibu wa sheria ya sensa kifungu namba 43(3) ambacho kinaeleza makosa ambayo raia hapaswi kuyafanya .

HABARI KUBWA KATIKA JARIDA LA LUDEWALEO JUNI 02, 2022

Habari kubwa katika Jarida letu la leo ni jengo la Ofisi kubwa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Ludewa linalo jengwa katika Halmashauri hiyo huku ujenzi wake ukiendelea kwa kasi ukilinganisha na kipindi kilicho pita kwa sababu ya mvua kubwa zilizo kuwa zikiendelea kunyesha.

Kukamilika kwa jengo hilo litatatua kero ya ukosefu wa Ofisi za idara mbalimbali zilizotawanyika.

Lakini pia Ukamilikaji wa jengo hilo litakuwa ni jengo zuri ambalo litawavutia watu wengi kuja kulitembelea kutokana na uzuri wa jengo lenyewe na wengi watatamani kupiga picha katika eneo hilo.

Aidha katika jarida letu la leo habari kubwa iliyo gusa mioyo ya watu wengi ni kutoka pale Kata ya Luana ambapo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg.Sunday Deogratias aliwaahidi wananchi wa Kata ya Luana  alipo kuwa akiwahutubia katika mkutano wa wawazi na kusema kuwa, Kata ya Luana ni miongoni mwa kata zinazo fanya vizuri haswa katika ukelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasà, Ujenzi wa vituo vya afya nk.

Hivyo kwa uunga mkono jitihada za wananchi wa Kata hii sasa nikiwa Kama Mkurugenzi nitatoa Bati 176 ambazo Mhe. Diwani Wilbard Mwinuka ameniomba.

Hivyo nawaombeni wananchi tuendelee kuiunga mkono serikali yetu kwa kuendelea kufanya kazi ili tutekeleze miradi yote inayo endelea kwenye kata hii "alisema Sunday Deogratias Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Ludewa" kauli hiyo aliitoa Mei 29, 2022.

Licha ya Miradi mingi inayo tekelezwa kwenye Wilaya ya ludewa, Diwani wa Kata ya Ludende  Mhe. Vasco Mgimba akishirikiana na wananchi wa Kata hiyo wamefanikiwa kuinua jengo la Mama na mtoto la kituo cha Afya cha  Ludende ambao Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ilitia mkono wake kuunga mkono juhudi za wananchi, lakini pia Diwani wa Kata hiyo bado amenyenyekea chini ya serikali kuomba kuungwa mkono ili kukamilisha jengo hilo ambapo awali serikali ilitupia mkono wake katika hengo hilo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Ludewa bado amewapa Imani kubwa wananchi wa Kata hiyo kwa kusema kuwa,

Serikali inatambua mchango mkubwa wa wananchi wa Kata hiyo ndio maana Walipo omba Halmashauri isaidie kwa awamu ya kwanza ilitekeleza na kwasasa Mhe. Diwani kaomba tena na sisi Kama Halmashauri tutaaungana na wananchi kukamilisha jengo hilo kwa Bajeti ya Mwaka 2022/2023.

Katika hatua nyingine katika jarida letu la leo Juni 02, 2022 Sehemu ya juu inaelezea Ujenzi wa chuo cha Ufundi VETA kinacho jengwa Kata ya Lugarawa pale shaulimoyo, ujenzi wake unaendelea na kwasasa upo kwa asilimia 20% ambapo ukamilikaji wake ni  mwishoni mwa mwaka huu, na kusuasua kwa mradi huo ni kutokana na mvua kubwa zilizo nyesha kwa kipindi cha mwezi January hadi Aprili.

Pia neema nyingine yamwagika tangu kuumbwa kwa ulimwengi barabara ya kutoka Mbwila hadi Lifuma inaendelea na uchimbwaji ambapo kukamilika kwa barabara hiyo itakuwa imeokoa gharama kubwa za usafiri ukilinganisha na wakati huu wananchi hulazimika kusafiri kwa kutumia Ziwanyasa (Mitumbwi na Boti)

Jitihada za Mhe. mbunge wa Ludewa  Joseph Kamonga zinaendelea kuzaa matunda, na ikumbukwe kwamba Jana Mei moja aliweza kuhoji Bungeni mambo mbalimbali ikiwemo uendelezwaji wa nguvu

za wananchi wake.