Saterdag, Februarie 10, 2018

Serikali yawasha moto Bungeni kuhusu madanguro, biashara ya ngono


Serikali imesema ina andaa mikakati itakayowezesha kudhibiti biashara ya ngono na uwepo madanguro nchini, hasa kwenye maeneo ya mijini.

Vrydag, Februarie 09, 2018

RC,RUKWA APIGANA NA PANYA




Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbwanga Dk. Khalfan Haule kuhakikisha anatafuta dawa ya kuulia panya wakiwa mashambani ili kuokoa miti kutokana na uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya.

Shahidi akana kuona mkojo wa Wema Sepetu

Kesi ya msanii  Wema Sepetu ya kukutwa na msokoto wa bangi imesikilizwa jana February 8, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Inspekta wa Polisi, Wille aliieleza Mahakama kuwa hakuwepo wakati Wema akichukuliwa sampuli ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa serikali.

Donderdag, Februarie 08, 2018

Sakata la Msamaha wa Babu Seya na Mwanaye Laibuka Bungeni

Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya (CUF) Mhe. Abdalah Mtolea ameibua sakata la kusamehewa Babu Seya na mwanae, Johnson Nguza 'Papii Kocha' na kusema halikuwa jambo jema kwa kuwa watu hao mahakama iliwabaini kuwa ni wabakaji.

Meneja wa Diamond Amtolea Uvivu Ruge Mutahaba wa Clouds Media

Meneja wa label ya WCB, Sallam SK amefunguka kwa kuendelea kudai kw Fmamba kampuni yao haina tatizo na chombo chochote cha habari isipokuwa Ruge Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Clouds FM na Clouds TV ndio mwenye tatizo na label hiyo.

WAZIRI MAJALIWA AWAPINGA CHADEMA

Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa amesema hajui kama kuna kata ambayo mgombea wa Chadema ilishinda lakini hakutangazwa, badala yake akatangazwa mshindi kutoka chama kingine cha siasa.

Ametoa kauli hiyo leo Februari 8, 2018 bungeni Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu (Chadema), Devotha Minja.

Katika swali lake, Minja ametaka kujua Serikali inasema nini kuhusu ukandamizwaji wa haki unaofanywa na wasimamizi wa uchaguzi ambao wanawatangaza wagombea ambao hawakushinda na kuwaacha walioshinda.

Mbunge huyo ametoa mfano wa Kata ya Sofi mkoani Morogoro ambako mgombea wa Chadema alipata kura 1908, wa  CCM kura 1878.

Pia, ametaja Kata ya Siyui mkoani Singida, mgombea wa Chadema alipata kura 1,358 huku wa CCM akipata kura 1304, lakini waliotangazwa wote walikuwa wa chama tawala.

Katika majibu yake, Waziri Majaliwa amesema hatarajii kuwa tume inaweza kuwatangaza walioshindwa na kuwaacha washindi.

"Lakini sheria zinaipa nafasi Tume  ya Uchaguzi (NEC) kukutana na vyama vinavyogombea ili kuwapo na nafasi ya kujadiliana kwenye upungufu," amesema Majaliwa.

Hata hivyo, amewataka wanaohisi kuonewa waende mahakamani kudai ushindi wao katika kipindi kisichozidi miezi mitatu ili sheria itazamwe kwenye ushindi huo.


Chrispiny kalinga blog

Majibu ya Serikali Kuhusu Zile Milioni 50 Ilizoahidi Kwa Kila Kijiji


Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi amesema kuwa serikali itaweka utaratibu utakaowezesha kutekelezwa kwa ahadi ya kutolewa milioni 50 kila kijiji, hivyo wananchi wasiwe na hofu.

Jaji Mkuu Aionya Serikali



Jaji Mkuu nchini Kenya David Maraga, ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi hiyo katika kukabiliana na upinzani.

 Jaji Maraga ametoa kauli hiyo ikiwa imepita masaa kadhaa tokea kufukuzwa kwa mwanasheria maarufu ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia kuapishwa Raila Odinga katika uwanja wa ‘Uhuru Park’ kufukuzwa nchini humo na kupelekwa Canada.

Katika ukurasa wake wa Twitter Jaji Maraga amesema malalamiko yaliyopelekwa Mahakamani yalikuwa wazi na majukumu ya kufanyia maamuzi yalikuwa ya Mahakama kutokana na kwamba ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe.

Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya Kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama

View image on TwitterView image on Twitter
Please see my Statement on failure to comply with court orders.
Chrispiny kalinga blog

WAFANYAKAZI NJOMBE WAUZWA KUSIKO JULIKANA


KIBENA

Wafanyakazi wa kiwanda  cha chai cha kibena wilayani Njombe Mjini katika Mkoa wa Njombe wanaulalamikia Uongozi wa Kiwanda hicho kwa madai hawatendewi haki stahiki zinazo takiwa kutendewa kwa mujibu wa sheria za kazi.


katika barabara ielekeayo makambako na hapa ni barabarani  kwenye kibao cha kuelekea kwenye kiwanda cha chai kiitwacho kibena tea ltd

Woensdag, Februarie 07, 2018

USHIRIKINA WAINGIA SHULENI LUDEWA, WATOTO WAPELEKWA SHAMBANI



Mwandishi wetu Ludewa

Tatizo la kuanguka mara kwa mara kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muholo iliyopo katika Kijiji cha Muholo kata ya Luana Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Iimeilazimu kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Ludewa Ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ambae ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere Kufika katika Kijiji Hicho ili Kubaini Tatizo.