Dinsdag, Januarie 30, 2018
Je wajua waweza kupata faida nyingi toka kwa nyuki?
Kilimo Bora Cha Karoti
Karoti ni zao la mbogamboga ambalo ni zao la jamii ya mzizi, kwa
kawaida hupatikana katika rangi ya machungwa, zambarau, nyeusi,
nyekundu, nyeupe na njano. pia zinafaida kubwa katika mwili kwa
kukupatia vitamin A na C pamoja na madini ya chuma. Lakini pia asili ya
zao hili ni Persia – Ulaya na kusini magharibi mwa Asia. Kwa Tanzania
zao hili hulimwa hasa mikoa ya Iringa, Mbeya, Morogoro, Arusha, Kagera
na Kilimanjaro.
Hali ya hewa na udogo ifaayo kwa kilimo hiki.
Karoti zinahitaji hali isiyokuwa na joto sana, wala baridi sana, kati ya nyuzi za degree 15 mpaka 27 za sentigredi. Kama ukanda wa pwani una joto kali, inatakiwa karoti zilimwa miezi ya majira ya baridi, karoti zinazotoka mazingira ya baridi huwa na radha nzuri pamoja na harufu nzuri ukilinganisha na karoti zinazolimwa kanda zenye joto. Udongo wa kichanga chepesi na tifutifu ndio unafaa katika kilimo cha karoti, udongo wa mfinyanzi na udongo mzito hudumaza mazao.
Hali ya hewa na udogo ifaayo kwa kilimo hiki.
Karoti zinahitaji hali isiyokuwa na joto sana, wala baridi sana, kati ya nyuzi za degree 15 mpaka 27 za sentigredi. Kama ukanda wa pwani una joto kali, inatakiwa karoti zilimwa miezi ya majira ya baridi, karoti zinazotoka mazingira ya baridi huwa na radha nzuri pamoja na harufu nzuri ukilinganisha na karoti zinazolimwa kanda zenye joto. Udongo wa kichanga chepesi na tifutifu ndio unafaa katika kilimo cha karoti, udongo wa mfinyanzi na udongo mzito hudumaza mazao.
Lita 85 za Gongo zakamatwa Manyara
Sh 1.1 Tirilioni zatolewa kusaidia mapambano dhidi ya Malaria
Kampeni za Kinondoni CHADEMA, CCM wazidi kutifuana
Sumaye Ampa Makavu Mtulia.....Awataka Wananchi Wampuuze
Waziri
Mkuu Mstaafu , Frederick Sumaye amefunguka na kusema kuwa kazi ya
Mbunge ni kutetea wananchi wa jimbo lake na si kwenda kumsifia Rais na
kudai wabunge waliojizulu nafasi zao kwa kigezo cha kumuunga mkono Rais
hawakutambua majukumu yao.
Sumaye
amesema hayo kwenye kampeni za Ubunge wa marudio katika jimbo la
Kinondoni zinazoendelea na kusema kuwa kwa Wabunge ambao wamejiuzulu
nafasi zao na kwenda chama kingine kugombea tena hawafai kabisa kuwa
wabunge kwa kuwa hawatambui maana ya Ubunge.
"Kazi
ya Mbunge si kwenda kumtetea Rais bali ni kutetea wananchi waliompa
kura, kama Mtulia yeye anasema ameondoka na kudharau kura za watu wa
Kinondoni kwa sababu amependezeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania basi akateuliwe na Rais kuwa Mbunge maana kazi yake ndiyo
itakuwa kwenda kumtetea na kumsifia Rais.
"Watu
ambao wanahama chama eti kwa sababu Rais ametenda mambo mema pamoja na
ukweli kwamba mimi naweza kubishana sana maana hatujaona hayo mambo wewe
kama umehama maana yake ulikuwa huelewi maana ya kuwa Mbunge"
alisisitiza Sumaye
Mbali
na hilo Sumaye alidai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sasa hakijali
tena maslahi ya wananchi wake kwa kuwa kimeshika madaraka kwa muda mrefu
ndiyo maana wameweza kumrudisha Mtulia kugombea kwenye jimbo la
Kinondoni bila kujali mtu huyo amesababisha fedha za wananchi zaidi ya
bilioni moja ziteketee kwenye uchaguzi wa marudio wakati fedha hizo
zingeweza kutumika katika kufanya mambo ya maendeleo kwa wananchi.
chrispiny kalinga Jambo muhimu la kuzingatia katika kutimiza ndoto zako
Leo
nimejikuta namkumbuka sana mwalimu wangu wa somo la Kiswahili, moja
kati ya vitu ambavyo vimenifanya niweze kumkumbuka ni vile ambavyo
alikuwa anajitoa kwa hali na mali katika kuhakikisha tunaelewa somo la
Kiswahili. Ni siku nyingi kidogo zimepita lakini kile ambacho
alinifundisha bado hakijafutika akili mwangu, na sina uhakika kama
kitakuja kufutika.
Mwalimu wangu huyu sitachoka kumuombea kwa mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo analifanya aweze kufanikiwa Zaidi. Namkumbuka kwa sababu kuna somo ambalo alitufundisha kwa kutumia nguvu zote, somo hili ni somo la nyakati.
Mwalimu wangu huyu sitachoka kumuombea kwa mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo analifanya aweze kufanikiwa Zaidi. Namkumbuka kwa sababu kuna somo ambalo alitufundisha kwa kutumia nguvu zote, somo hili ni somo la nyakati.
Wakazi Wa Dar Wamiminika Ofisi za Mkuu Wa Mkoa Kujua Hatima Yao
Zaidi ya Wananchi elfu tatu leo wamejitokeza ikiwa ni Siku ya kwanza ya Utatuzi wa Malalamiko ya Kisheria kwa Wananchi waliodhulumiwa chini ya Wanasheria Magwiji 160 ikiwa ni Mkakati wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kusaidia wanyonge waliodhulumiwa Mali zao kupata haki pasipo kuvunja sheria.
Wananchi hao wametaabika kwa muda mrefu baada ya kudhulumiwa Mali zao Walizochuma kwa Tabu na sasa kupitia huduma ya Masada wa kisheria uliotangazwa na RC Makonda wanaamni watarejeshewa haki yao.
Makonda amesema idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza leo inatoa picha kamili Kuwa wapo viongozi wasiotekeleza vyema majukumu yao ya kiofisi kwenye idara zao ambapo ameahidi kuwawajibisha.
Aidha Makonda amesema kilichomgusa kuandaa Wiki ya msaada wa kisheria ni baada kubaini uwepo wa wananchi wanaonyanyasiki na hata kufikia hatua ya kufa kwa presha au kupooza miili baada ya kudhulumiwa na watu wenye pesa au wanaotumia uelewa wa sheria kukandamiza wanyonge.
Kutokana na idadi kuwa kubwa wanaoendelea kujitokeza Makonda anaongeza wanasheria wengi zaidi ili kuhakikisha Kila anaefika na kupata namba anahudumiwa ipasavyo ambapo amewaomba wanasheria kuhakikisha wanawasikiliza wananchi kwa umakini na kuchambua nyaraka kwa ufasaha na wasitoe hukumu.
Makonda amesema katika zoezi hili limehusisha Wanasheria wabobezi, Wataalamu wa kutambua nyaraka zilizogushiwa, watendaji wa Ardhi na watumishi wa Mahakama ambao wapo kwaajili ya kuwahudumia Wananchi.
Pia Makonda amesema baada ya kupokea ripoti kamili ya kesi zote atasimama kuhakikisha Hakuna mnyonge anabaki akinyanyasika.
Zoezi la kusikiliza wananchi waliodhulumiwa Mali zao ikiwemo Nyumba, Viwanja, Magari, Mirathi na Kazi litaendelea hadi siku ya Ijumaa ya February 2.
Nao wananchi waliojitokeza wamemshukuru Makonda kwa kutambua Tabu wanazozipata baada ya kudhulumiwa na wajanja ambapo wengine wamesema wamepoteza Waume, Wake zao na wengine kupata magonjwa baada ya kudhulumiwa na wametaabika Muda mrefu kutafuta haki pasipo kufanikiwa lakini kupitia utendaji kazi makini wa Makonda wanaamni haki inapatikana
chrispiny kalinga
Maandag, Januarie 29, 2018
Basi la Tahmeed lawaka moto Tanga
Teken in op:
Plasings (Atom)