Woensdag, Januarie 31, 2018

Hii ndio gharama ya passport za kielektroniki

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.  Mwigulu Nchemba amesema kuwa gharama mpya ya hati ya kusafiria ya kielektroniki itakuwa Sh. 150,000.

Barnaba atoa siri kinachomuingizia mkwanja mrefu


u


STAA wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kipekee, Elias Barnaba amesema kuwa kitendo cha kuwatungia mastaa ngoma zao hasa wa kike kimemfanya kutengeneza mkwanja mrefu.

Shamsa apigwa stop kutumia Mitandao ya kijamii na mumewe


STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford anadaiwa kupigwa stop kutumia mitandao ya kijamii na mumewe, Chid Mapenzi na kwa muda sasa haonekani hasa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambako aliwaaga kabisa mashabiki zake.

Madee azungumzia bifu lake na Roma


BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hitmaker wa Ngoma ya Sema, Hamadi Ally ‘Madee’ hatimaye amefungukia kile kinachodaiwa kuwa ni bifu zito lililopo kati yake na msanii mwenzake, Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Madee alisema suala la uwepo wa bifu kati yake na Roma ni hisia tu zinazo-zushwa na mashabiki kutokana na vijembe wanavyo-tupiana na msanii huyo ambaye kimsingi ni mtani wake.

“Roma ni mtani wangu, mara nyingi huwa kuna masihara kati yangu na yeye, hata familia yake kwa ujumla, vile vijembe ambavyo huwa tunatupiana ule huwa ni utani tu hakuna uhalisia wowote, hatuna bifu kati yetu,” alisema Madee


chrispiny kalinga

Tanesco yapewa agizo



NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amelitaka Shirika la Umeme (Tanesco) mkoa wa Kilimanjaro kuweka mkandarasi wa kusimamia miradi ya umeme vijijini kila wilaya, ili ikamilike kwa wakati ifikapo Aprili, mwakani.

Jafo atoa agizo madarasa ya nyasi, udongo



SERIKALI imewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha wanaondoa madarasa ya tembe, nyasi na udongo kwenye maeneo yao.

Marufuku michango ya Elimu yazua mjadala kwa Viongozi


UAMUZI wa Rais John Magufuli kupiga marufuku michango ya elimu katika shule za msingi na sekondari, umezua mjadala katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Kahama mkoani Shinyanga.

Kijiji chavamiwa na kundi kubwa la Fisi



WANANCHI wa Kata ya Inyeze wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamelalamika kwa diwani wa kata hiyo kwa kuvamiwa na kundi kubwa la fisi  kijijini.

Viongozi wengine waliowahi kuapishwa na kujitangaza kuwa marais kama Odinga barani Afrika

 Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga Jumanne aliapishwa kuwa 'rais wa wananchi' nchini humo baada ya kusema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini humo Oktoba mwaka jana.

Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper hakujitokeza kwa sherehe hiyo ya kuapishwa, ingawa alikuwa miongoni mwa waliotarajiwa kuapishwa.

Waziri mkuu huyo wa zamani hayuko peke yake katika kujaribu kujitangaza marais, kukiwa bado kuna rais mwingine madarakani.

Wengine ni akina nani?
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Etienne Tshisekedi, Nigeria Moshod Abiola, Uganda Kiza Besigye na Jean Ping wa Gabon ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wa Afrika ambao wamejaribu kujitangaza kuwa marais, na sasa Raila Odinga amejiunga na orodha hii.

Etienne Tshisekedi

Nyumba ya kiongozi wa upinzani yapigwa bomu


Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya ambaye sasa ni kiongozi mwenza wa NASA, Stephen Kalonzo Musyoka nyumba yake imepigwa bomu usiku wa kuamkia leo katika eneo la Karen, Nairobi Kenya na watu wasiojulikana.

Waliovua nguo kortini jela miezi 6


Washtakiwa 24 kati ya 61 wanaokabiliwa na kesi za ugaidi jijini hapa wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kuvua nguo, kisha kugoma kuingia ndani ya chumba cha mahakama kusikiliza kesi zao.

Watanzania Mil 25 wadaiwa kukosa msaada wa sheria


 
Wananchi zaidi ya milioni 25 nchini Tanzania wamedaiwa kuwa hawapati huduma za kimahakama kutokana na upungufu wa majengo ya mahakama na uhaba wa watumishi hususani kwenye mahakama za mwanzo.

Takwimu hiyo imebainika hapo jana  katika uzinduzi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo wakati Jaji Mkuu wa

Wanawake wawili kuuawa kwa kukatwa mapanga kutokana na imani za kishirikina.


Watu watatu wameuawa katika matukio tofauti likiwamo la wanawake wawili kuuawa kwa kukatwa mapanga kutokana na imani za kishirikina.