Donderdag, Augustus 09, 2018

Diamond Platnumz, Ang'ang'ania Kubeba Jeneza la Mzee Majuto

































mubashara blog

+255753121916

Mbunge Ester Matiko, Mwandishi wa Tanzania Daima na Wafuasi wa CHADEMA Waachiwa Baada ya Kukamatwa jana na Polisi

Mbunge wa Tarime Mjini,  Ester Matiko, mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima Sitta Tuma na wafuasi wengine 14 wa Chadema waliokuwa wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mkutano usio halali wameachiwa. Hata hivyo, wametakiwa kuripoti polisi kesho.

Rais Magufuli Ashindwa Kujizuia na Kumwaga Machozi Akimuaga Mzee Majuto

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameshindwa kujizuia na kujikuta akimwaga machozi wakati alipokuwa akiaga mwili wa aliyekuwa msanii nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Agosti 9, 2018.

Woensdag, Augustus 08, 2018

Mwanafunzi miaka 8 abakwa asababishiwa ugonjwa



Mwanafunzi (8) wa darasa la kwanza wa shule ya msingi Maganjwa Wilayani Babati, Manyara (jina linahifadhiwa) amebakwa na mkazi wa Kijiji hicho na kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri hali iliyomsababishi ugonjwa wa Fistula.

Waziri agoma kuwasha umeme, mkandarasi nae matatani



Wananchi mkoani Rukwa wamelalamikia kasi ndogo, inayofanywa na mkandarasi wa kusambaza umeme wa mradi wa umeme vijijini wa REA, ambapo kati ya vijiji 142 vilivyopangwa kupitiwa na umeme huo kwa awamu ya tatu, ni vijiji saba tu vilivyofikiwa hadi sasa na kwa wateja wasiozidi kumi tu.

Nay Wa Mitego - Mwaka Wa Roho Mbaya (Official Video) hii hapa

































mubashara blog

+255753121916

CCM Yalalamika Siri za Serikali Kuvuja

Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Dk. Antony Dialo amesema miongoni mwa matatizo ambayo watumishi wengi wanaostaafu au kuondolewa katika nafasi wanazoteuliwa na Rais ni kukiuka kiapo chao cha kutunza siri.

Nay wa Mitego aachia ngoma mpya ‘Mwaka wa Roho Mbaya’

Rapa Ney wa Mitego ameachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Mwaka wa Roho Mbaya’ ambapo kwenye mashairi ya wimbo huo kafunguka mambo kibao ikiwemo Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

Walinzi Wauana kwa Risasi kisa deni la Sh. 30,000

Mlinzi  wa kampuni ya Lake Security, ameuawa kwa kupigwa risasi tumboni na mlinzi mwenzake baada ya kuzuka ugomvi kati yao wa kudaiana Sh. 30,000.

WCB yawapatia magari wasanii wake Lavalava na Mbosso

WCB yawanunulia magari wasanii wake, Mbosso na Lavalava hii ni mara baada ya Diamond Platnumz kuposti video clip kwenye Insta Story yake na kuonesha magari hayo hapo jana siku ya Jumanne.

NEC Yaijibu CHADEMA Kuhusu Uchaguzi Mdogo Jimbo La Buyungu




Hussein Makame-NEC
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia amesema Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Buyungu ataendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuwa malalamiko yaliyotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kumkataa msimamizi huyo hayakufuata taratibu za kisheria.

Dinsdag, Augustus 07, 2018

Benki kuwakopesha wavuvi zana



BENKI ya Wananchi Tandahimba (Tacoba) mkoani Mtwara, imesema inatarajia kuwakopesha wavuvi ili kuongeza mtaji na kuboresha shughuli zao na hatimaye kuchangia pato la taifa.

Tetemeko la ardhi latokea Rukwa na Congo

 

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa  kipimo cha ritcher 4.4 na kina cha Kilomita 10 limetokea katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Rukwa na maeneo ya jirani usiku wa kuamkia leo Agosti 7, 2018