BENKI ya Wananchi Tandahimba (Tacoba) mkoani Mtwara, imesema inatarajia kuwakopesha wavuvi ili kuongeza mtaji na kuboresha shughuli zao na hatimaye kuchangia pato la taifa.
Ofisa Maendeleo ya Biashara wa Benki hiyo, Said Nambecha, alisema hayo juzi kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Wakulima (Nanenane) Kanda ya Kusini yanayoendelea mkoani Lindi.
Nambecha alisema hayo baada ya kuulizwa swali juu ya kundi hilo kusahauliwa katika uwezeshaji ikiwamo taarifa zilizoenea kwamba wavuvi wamekuwa hawaaminiki hivyo kutopatiwa huduma hiyo.
Alisema mara nyingi taasisi zinasita kuvipatia mikopo vikundi vya wavuvi kutokana na kazi zao kuwa na vyombo wanavyovitumia kupotea kwa kuzama na wao wenyewe kupoteza maisha. Alisema jambo hilo huzipa hofu taasisi za fedha namna ya kurejeshwa.
“Hii ni moja ya sababu zinazozifanya benki nyingi kusita kuwakopesha wavuvi,” alisema Nambecha.
Nambecha alisema kutokana na umuhimu wa sekta hiyo, Tacoba inaangalia utaratibu utakaohakikisha kundi hilo linakopeshwa vifaa badala ya fedha.
Pia alisema samaki ni moja ya bidhaa zinazopendwa na kuhitajika kwa wingi kwa matumizi ya binadamu sambamba na kuwa na soko kubwa kiasi cha wavuvi kurejesha kwa urahisi mikopo yao, tafauti na wateja wengine.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking