Saterdag, Augustus 25, 2018

JINSI AMBAVYO UNAWEZA KUTUNZA PENZI LAKO KWA MWENZI WAKO


ASANTE
Wiki iliyopita tulijifunza namna ambavyo unaweza kuanzisha mahusiano na mtu yeyote unaye mpenda....mimi naitwa chrispin kalinga ambaye nakusogezea kila wiki lakini unayo nafasi ya kunitafuta kwa simu yangu ya mkononi :0753121916

basi twende sambamba kwa kujifunza namna ambavyo mahusiano yanavyo anza,,,,,,,,,,,,,

Kwa kawaida, uhusiano huanza pale mtu anapovutiwa na mwingine iwe kihisia au kimwili. Hiyo ndiyo hatua ya kwanza kabisa ya mahusiano ambayo hutegemea masuala makuu mawili.

Jambo la Kwanza kabisa, ni ukaribu, Tunaambiwa kwamba, watu wawili wanapojikuta bila hata wao wenyewe kutarajia katika mazingira ya ukaribu iwe kwa kufanya  kazi ofisi moja au kuabudu mahali pamoja, kusoma mahali panapofanana au kuishi mtaa mmoja, huongeza uwezekano wa mmoja wao kuvutiwa na mwenzake na hivyo kuanzisha mahusiano.

Tafiti nilizo zifanya nikapata majibu kuwa kadri unavyokutana na mtu iwe kwa kumwona na kumsikia mara kwa mara, ndivyo unavyoongeza uwezekano wa kumpenda  na  kawaida, hatuvutiwi na vitu tusivyojua kwa karibu ikiwamo watu. Kwa maana nyingine, kadri unavyokutana na mtu ndivyo unavyojikuta ukiongeza nguvu ya kumpenda.

Kwa upande mwingine, ukaribu huu huongeza uwezekano wa kufanana mambo fulani fulani kama imani na mitazamo na hivyo kuongeza ukaribu. Mfano, vijana wanaokutana kanisani mara kwa mara kwenye ibada, mbali na kuongeza uwezekano wa kuvutiana, lakini pia huongeza uwezekano wa watu hao kuwa na imani, mitazamo na tabia  zinazofanana. Haya matatu huwa ni kichocheo cha mvuto unaojenga mawasiliano ya kimapenzi.
Kwa kawaida, watu hujenga uhusiano na wale wanaowafanya wajisikie vizuri, yaani wanao wafanya wajisikie  kuwa na furaha na Amani. Na kadri mtu anavyojisikia vizuri, ndivyo anavyo vutiwa na wewe. Kinyume chake, ni kujisikia mzigo na hivyo kuongeza uwezekano wa mahusiano kwenda mbele. Kwa mfano, mwanamke hujisikia vizuri anapokuwa na mtu anaye mfanya ajisikie kuwa mzuri na wa maana kama tulivyoona.Jambo la pili msomaji wangu na msikilizaji wangu linaloanzisha mahusiano ni mvuto wa kimwili. Hapa tunazungumzia uzuri wa sura, urefu/ufupi, unene/wembamba, weupe/weusi na kadhalika. Sasa, uzuri  nao unachangia.  Watu wanatofautiana namna wanavyo tafsiri uzuri kutegemeana na utamaduni, malezi, imani na sababu nyinginezo. Na wakati mwingine, uzuri wa mtu hutegemea pia 'viwezeshi' ninapo sema viwezeshi ninamaana ya malezi;kama mavazi, mapambo, anavyozungumza, anavyotazama na kadhalika.

Vyovyote vile iwavyo, wengi wetu huamini mtu mwenye mwonekano mzuri  tunaouona sisi kuwa ni mzuri, basi automatically huwa na haiba na tabia njema. Tuna mazoea ya kuhusianisha uzuri unaoonekana na uzuri usioonekana. Ni aina fulani ya stereotype yenye misingi yake kwenye malezi. Kwamba mzuri ana tabia nzuri jambo ambalo hutufanya tutamani kuhusiana na watu tunaowachukulia kuwa wazuri.

Hata hivyo, tunaambiwa, pamoja na kwamba watu wengi hutamani kujenga mahusiano na watu wenye mwonekano mzuri wa kimwili, mara nyingi huishia kujenga mahusiano na watu wenye mvuto unaolingana na mvuto walionao wao wenyewe. Unajikuta unahusiana na mtu anayefanana na wewe kwa kiasi fulani. Ni hivyo mara nyingi. Ndio kusema, wanaotamani kuhusiana na watu fulani wenye uzuri wa viwango fulani, hujikuta wakihusiana na watu wa kawaida kama wao. 

Bahati mbaya ni kwamba, mwonekano wa mwili huwa na nafasi kubwa katika hatua za mwanzo za uhusiano na kuwa mahusiano ya kudumu huwa hayategemei mvuto kama nitakavyoelezea katika aya chache zinazofuata. Lakini pamoja na matatizo yake, uzuri wa sura na umbo una nafasi yake, kubwa tu, ya kumfanya mtu ajiingize kwenye mahusiano.

MAMBO YANAYOENDELEZA MAHUSIANO MAPYA

Wataalam wa mahusiano wanatuambia, baada ya mtu kuvutiwa na mtu fulani, ni kawaida mtu huyo kufanya juhudi za kumvutia mtu huyo kwa kujaribu kujenga taswira chanya ili naye avutiwe naye. Kanuni nne kubwa zinazosaidia kuwafanya watu wawili waanze kuwa karibu kihisia, ili waweze kuhusiana bila mikwaruzo,wala pingamizi, ni haya yafuayo:
·         Watu wana kawaida ya kukupa kile unachowapa, hivyo mtu anayeonesha kuvutiwa na sisi, hutufanya tujisikie kuvutiwa nae na kutamani kutumia muda mwingi nae. Tunajisikia kuchoka tunapo mpenda asiyeonesha kutupenda. Kwa hiyo mtu humpenda zaidi yule anaye mpenda na yeye.
  • Watu unaofanana nao imani, mitazamo na misimamo hupendana zaidi kuliko wale wanaotofautiana imani, mitazamo na misimamo. Kufanana kunakoambatana na mvuto wa kimwili, huchochea mvuto, na mvuto huo huchochea kufanana. Hata hivyo, watafiti wanasema, zipo tofauti za kihaiba ambazo kwa kawaida huchochea kuvutiana. Mfano mtu mzungumzaji hujisikia kuvutiwa  na mtu anayeweza kumsikiliza na si yule anayetaka kuzungumza kama yeye.

  • Lakini pia Kumwamini unayevutiwa naye, humfanya avutike kwako. Hii hutegemea kiwango cha usalama wa kihisia  unacho kuwa nacho wewe na kiwango hicho hicho cha usalama anachokuwa nacho yeye. Kutokuwa salama kihisia  kunamaanisha ama kutokujiamini, kutokuamini wengine au vyote viwili, ambavyo huathiri kwa kiasi kikubwa uhusiano. Lakini kwa kifupi, nafsi isiyosalama, hushindwa kuamini na hivyo hupunguza kumvutia mwingine.



mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking