Saterdag, Augustus 04, 2018

Waziri Kingwangalla kuhamishiwa hospitali ya KCMC kwa helkopta

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla leo Jumamosi Agosti 4, 2018 amepata ajali eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini. Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba amefariki dunia.

Mwenyekiti wa jumuiya ya hifadhi ya jamii  ya Wanyamapori ya Buruge (WMA), Ramadhan Ismail amesema waziri huyo anapatiwa matibabu katika kituo cha afya Magugu.

Amesema baada ya kupatiwa matibabu katika kituo hicho cha afya, helkopta imefika eneo hilo tayari kwa kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu zaidi.

Amebainisha kuwa Dk Kigwangalla ana maumivu katika mbavu, kiunoni na hawezi kutembea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augostino Senga amesema katika gari hilo alikuwepo Dk Kigwangalla, dereva wake, mwandishi wa habari, msaidizi wake na mlinzi.

Amesema hali ya waziri huyo inaendelea vizuri licha ya kuwa ameumia mkono wa kulia, kifua na shingo


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking