Wanachama
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli wameandamana kwenye
ofisi za chama hicho wakitaka aliyekuwa Mbunge wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo(CHADEMA), Julius Kalanga aliyejiunga na chama hicho kufuata
utaratibu ikiwemo hatua za uteuzi wa nafasi ya kugombania ubunge.
Aidha,
Wakizungumza katika Ofisi hizo wamesema kuwa wamesikia taarifa za
kuteuliwa kwake bila kufuata utaratibu ikiwemo kukaa vikao na wazee wa
kimila Malaigwanani ili waweze kumpitisha.
Hata
hivyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Monduli amesema kuwa hajashiriki
kwenye vikao na wazee wa kimila kama inavyodaiwa na baadhi ya wanachama
hao na kwamba utaratibu utatumika katika kuwapata wagombea
“Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinataratibu zake, kina katiba, sheria ambazo zote
zitafuatwa katika mchakato huu wa kumpata mgombea ubunge wa jimbo hili
la Monduli,”amesema mwenyekiti wa chama wilaya ya Monduli, Wilson
Lengima
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking