Watu
13 wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi
ya uhujumu uchumi ikiwemo utakatishaji fedha wa Shilingi Milioni 154.
Akiwasomea
mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kelvin Mhina wakili wa
serikali mkuu, Nassoro Katuga amedai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na
mashtaka 5 ambayo wameyatenda katika mikoa tofauti.
Katika
kosa la kwanza la kula njama ya kutenda kosa linawakabili washtakiwa
wote ambapo wanadaiwa wamelitenda kati ya March 2018 na June 2018 katika
jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Rukwa na katika maeneo mengine ya
Jamhuri ya Tanzania.
Pia
kosa jingine ni kusambaza taarifa za uongo kupitia mfumo wa kompyuta
ambapo wanadaiwa wamelitenda March na June 2018 wakiwa Dar es Salaam na
Rukwa ambapo walichapisha taarifa fupi za jumbe (Message) ili kujipatia
kitu.
Wakili
Katuga amedai kosa jingine ni kusambaza jumbe (message) kwa njia ya
Elektroniki kati ya March na June, 2018 kwa nia ya kudanganya na
kushawishi kati ya Dar es Salaam na Rukwa walisambaza kwenda kwa watu
tofauti tofauti ili kuonyesha wana mamlaka hayo.
Pia
katika kosa jingine la kusambaza jumbe fupi za Kielektroniki, wanadaiwa
walilitenda March na June, 2018 kati ya Dar es Salaam na Rukwa
walisambaza jumbe zisizotakiwa kwa njia ya Kielektroniki.
Katika
kosa la mwisho wanadaiwa ni utakatishaji fedha ambapo wanadaiwa
wamelitenda kati ya March na June 2018 katika maeneo ya Dar es Salaam na
Rukwa.
Inadaiwa
kwa pamoja walijihusisha katika ufanyaji wa muamala wa Sh.Mil
154,032,830 ikiwa ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Katuga amedai upelelezi haujakamilika
ambapo Hakimu Mhina amesema kesi hiyo haina dhamana kwa sababu ni ya
uhujumu uchumi, hivyo wataenda rumande ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi
August 21,2018.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking