Na. chrispin kalinga.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Mabodi amewataka Wabunge na Wawakilishi nchini kuongeza kasi ya kutatua kero za wananchi kwa wakati kama walitoa ahadi zao katika uchaguzi mkuu uliopita.
Wito huo ameitoa mara baada ya makabidhiano ya magari matatu katika jibo la kijito upele pangawe Zanzibar ambapo Magari hayo yana thamani ya shilingi milioni 128 yaliyotolewa na Mbunge wa Majimbo hayo, Shamsi Vuai Nahodha.
Akizungumza katika ziara yake ya kutembelea majimbo hayo iliyofanyika katika uwanja wa mpira wa Magirisi uliopo Kijitoupele, Dk.Mabodi alisema huu ndio wakati wa viongozi wa majimbo kutekeleza kwa kasi Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020.
Akizungumzia vitendea kazi hivyo ambavyo ni magari matatu yakiwemo mabasi ya Wanafunzi mawili na moja ambalo ni Canter kwa ajili ya shughuli za kijamii, aliwambia wananchi kuwa wanakiwa kuthamini juhudi za kiongozi huyo aliyetekeleza ahadi yake kwa vitendo.
Dk. Mabodi alieleza kwamba malengo ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha wananchi wa mijini na vijijini wanaondokana na changamoto mbali mbali za kijamii kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Alisema mabasi yaliyotolewa yatawasaidia wanafunzi wote wa majimbo hayo bila kujali tofauti za kisiasa.
kiongozi huyo A katika ziara yake ya kutembelea miradi mbali mbali ya Chama iliyokutekeleza ahadi walizowaahidi wananchi katika kampeni amesema wananchi wanakiamini na kukiunga mkono Chama kutokana na kutatua kwa wakati kero zinazowakabili wananchi.
“ Miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa majimboni na viongozi wa CCM ni kwa ajili ya wananchi wote, na tunaomba wananchi muendelee kutuamini na hatimaye mwaka 2020 mkichague Chama chetu kiendelee kuongoza dola.”, alisema Dk. Mabodi.
Naye Mbunge wa majimbo hayo, Shamsi Vuai Nahodha alisema CCM imeendelea kuwa na mvuto kwa jamii kutokana na ukweli na dhamira ya dhati ya viongozi wake kuwatumikia wananchi kwa vitendo.
Mbunge huyo Naohodha ambaye pia ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar alisema kwa kushirikiana na viongozi wengine wa majimbo mawili anayoyatumikia wamefanikiwa kutatua kero za wananchi kwa kiwango kikubwa.
Shamsi alisema na kuongeza kuwa wameimarisha huduma muhimu za kijamii zikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, ujenzi wa vituo vya Afya pamoja na ujenzi wa shule za kisasa za msingi na sekondari.
Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu pia alitembelea ujenzi wa Kituo cha Afya katika Jimbo la Kijitoupele ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa Mwakilishi wa jimbo hilo, Ali Suleiman Ali ‘’Shihata’’ pamoja na Mbunge wa jimbo hilo Shamsi Vuai Naohodha ambacho hadi kukamilika kwake kitatumia zaidi ya shilingi milioni 59.
Pia Naibu Katibu Mkuu Dk. Mabodi alitembelea Shule ya Sekondari Kwarara na Kituo cha elimu na habari sambamba na kukagua ujenzi wa shule ya msingi ya Kwarara itakayotumia shilingi bilioni 1.3 hadi ujenzi wake kukamilika
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking