CHRISPINY KALINGA
Twende
sambamba……..
Pamoja na imani kwamba mahusiano bora huwezekana kwa kukutana na mtu sahihi, tunaambiwa na watalaam wa mahusiano kwamba mwanamke yeyote anaweza kabisa kuwa na mahusiano na mwanaume yeyote kwa amani ikiwa kila mmoja wao atakuwa 'anamwamini au naweza sema kuaminiana ' na kujua mahitaji ya mwenzi wake
Lakini kabla sijaendelea zaidi, nikumbushie mambo makuu matatu yanayoanzisha mahusiano kwa maana ya kuwafanya watu wawili wapendane. Mambo hayo ni:
1) Hisia za kimapenzi au tamaa. Ingawa tamaa ina nguvu kubwa sana katika kuanzisha mahusiano, haiwezi kudumisha uhusiano huo kwa muda mrefu. Misingi ya hisia hizi za kimapenzi ni maumbile yanayoonekana.
2) Urafiki au ukaribu. unao jenga mazingira ya watu wawili kuwa karibu kihisia. Tunajifunza kuwa misingi ya ukaribu huu ni namna gani mahitaji ya kihisia ya mwenzi yanavyotambuliwa na kujibiwa bila kujali urafiki huo umetokana na tamaa au maamuzi na huu ndio msingi wa maamuzi.
3) Maamuzi ya kuweka ahadi. Ingawa kwa wengi dhamira ya kudumisha uhusiano hutokana na makubaliano ya awali, wakati mwingine, hutokea maamuzi hayo yakawa chanzo cha kuchipua kwa urafiki na hisia kama ilivyokuwa kwa wazee wetu wa zamani na Hiki ndicho kiwango cha juu cha uhusiano.
Sasa, ingawa uhusiano unaweza kuchipukia kokote kati ya tamaa, urafiki na maamuzi kutegemeana na imani, mitazamo na utamaduni wa wahusika, kilicho muhimu zaidi ni kile kinachofanyika baada ya uhusiano huo kuanzishwa ili kuufanya uendelee. Lakini Katika makala hii ninakufafanulia zaidi hari ya kuupeleka uhusiano huo .. Hiyo yote msikilizaji na msomaji wangu nilitaka tu kukuweka sawa ni kitu gani ambacho tunaendelea nacho katika mafundisho haya lakini kubwa zaidi ni kutembelea blog ya mubashara blog kwa taarifa na mafundisho mbalimbali sasa twende pamoja kwa kusoma na uelewe….
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking