Mwanafunzi (8) wa darasa la kwanza wa shule ya msingi Maganjwa Wilayani Babati, Manyara (jina linahifadhiwa) amebakwa na mkazi wa Kijiji hicho na kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri hali iliyomsababishi ugonjwa wa Fistula.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Augustine Senga amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Noeli Samweli na wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Dareda Joseph Lorri amesema amempokea mtoto aliyebakwa akiwa katika hali mbaya.
“Ameathirika kwa kiasi kikubwa sehemu za siri na hali hiyo imesababisha kupata ugonjwa wa Fistula,” amesema.
Amesema Daktari wa zamu alimpokea mtoto huyo hospitalini hapo Julai, 26, 2018 saa 3 usiku.
Kwa mujibu wa Lorri alibainisha kuwa mtoto huyo alitibiwa kwa kufanyiwa upasuaji na kushonwa ili kuunganisha sehemu za siri zilizochanika na hali yake inaendelea vizuri.
Mama(jina linahifadhiwa) anayemtunza mtoto huyo hospitalini hapo baada ya mama yake mzazi (jina linahifadhiwa) kuugua ghafla amesema kuwa wakati akimleta mtoto huyo haspitali alikuwa na majeraha mengine usoni na miguuni yaliyotokana na kun’gatwa na mbakaji huyo.
Amesema mtoto huyo alitumwa na mama yake kwenda kusaga majira ya saa kumi jioni lakini akiwa mashineni mtoto alirudishwa kwenda kuchukua Sh 250 na akiwa njiani kurudi nyumbani alikutana na Noel ambaye alimbeba na kumpeleka shambani na kumbaka.
Balozi wa kitongoji cha Maganjwa Baltazari Waree amesema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa ubakaji na kumfikisha kituo cha polisi Babati.
“Ni tukio la kinyama na linapaswa kulaaniwa na kila mtu na tunaiomba serikali ichukue sheria ili kuweza kukomesha vitendo kama hivi hususani kwa watoto wenye umri mdogo kama huyu,” amesema Waree.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking