Saterdag, Augustus 25, 2018

Zitto awajia juu wanaoponda muonekano wa wahudumu wa ATCL

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amekerwa na Watanzania wanaoponda muonekano wa wahudumu wa kike wa shirika la ndege la Tanzania (ATCL).

Zitto amesema kitendo hicho cha kusambaza picha mitandaoni sio kizuri kwani kinalenga kuwatukana, kuwadhalilisha na kuwanyayasa wahudumu hao ambao kwa kifupi ni watu ambao wamesomea taaluma hiyo.

“Nawaona baadhi ya Watanzania kwenye mtandao wa Twitter wakiwacheka wanawake wetu wanaofanya kazi ATCL. Kueneza picha hizo kwa lengo la kuwadharau/kuwatukana/ wanawake hawa ambao kiufupi wameseomea kazi hiyo hii ni aina ya unyanyasaji. Nimeshtushwa na kustaajabishwa sana. Ninawaomba Watanzania wenzangu wanaoutumia Twitter #TOT kuacha tabia hiyo,“ameeleza Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Baadhi ya Watanzania kupitia mtandao wa Twitter wamekuwa wakifananisha picha za wahudumu wa ATCL na wahudumu wa mashirika mengine makubwa barani Afrika.

Hata hivyo, sakata hilo limeibua mitazamo tofauti tofauti. Kwani kuna baadhi ya Watanzania wameunga mkono kuwa ATCL imeajiri wahudumu wa kike wasiokuwa na muonekano mzuri, wengine wakidai sare zao ndio mbaya ulinganisha na mashirika mengine.



mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking