Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amewataka wananchi wanaoishi Vijiji jirani vinavyopakana na machimbo ya madini ya tanzanite ya mereani wilayani simanjiromkoani manyara kusaidia kuwafichua watu wote watakaojaribu kuhujumu jitihada za serikali kudhibiti utoroshaji wa madini
Akizungumza na Wananchi wa Mji mdogo wa mererani mkuu wa mkoa wa njombe mh christoper sendeka amesema pamoja na suala la ulinzi wa rasilimali za nchi kuwa la watanzania wote walioko jirani na maeneo zinakopatikana wana wajibu mkubwa zaidi kwani pia lengo likitimia wanakuwa wa kwanza kunufaika .
Kwa upande wao baadhi ya wananchi Leopold Mao wamesema pamoja na hatua za kisheria zinazochukuliwa kulinda rasilimali za nchi yakiwemo madini kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu ya kuwawezesha wananchi kuwa wazalendo hasa waliko kwenye maeneo yenye rasilimali .
Ole Sendeka pia amekutana na kuwaomba viongozi wa kidini katika eneo hilo kusaidiana na serikali kuelimisha wananchi kuondokana na imani potofu watu kuwekeza katika ushirikina badala ya utaalam katika suala zima la utafutaji wa madini .
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking