Na James Timber, Mwanza
Kutokuwepo posho za watumishi wa serikali isiwe kikwazo cha kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo katika jamii kwani mtu mzalendo lazima ajitoe mhanga na aishi kisasa kama Ndege ya Dreamliner.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel katika Sikukuu ya Maenesho ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika eneo la Nyamhongolo jijini Mwanza, ambapo amewataka wahusika kuboresha eneo hilo liwe na hadhi ya kipekee kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa Magahribi, ambapo itawezesha wakulima na wafanyabiashara wawepo kipindi chote kwa lengo la kukuza uchumi.
"Naomba tumiliki eneo hili tulipe wananchi wanaotakiwa kulipwa fidia ila kama kuna mtu alikula fedha za wananchi tutamkamata, tukijenga uwanja huu utumike kwa miezi 12, huku tukitenga Siku Maalumu ya kusherekea Sikukuu hii lengo kubwa ni kukuza uchumi wa wafanyabiasha na Wakulima, nimepokea malalamiko kuwa utaratibu uliopangwa wa sikukuu ya mara moja kwa mwaka inawaumiza wakulima na wafanyabiashara sherehe zikiisha na biashara zao zinadolola," alisema.
Mhandisi Gabriel alitoa wito kwa watu wa mipango wajitahidi kufanya kitu cha kipekee ambacho kitakuwa mfano na mvuto katika eneo hilo, ambapo itawashawishi baadhi ya mataifa mbalimbali ya jirani kuja kujifunza na kununua bidhaa hapa nchini na kubainisha kuwa eneo hilo halina sifa kufanyia sherehe za sikukuu ya wakulima katika Serikali ya Awamu ya Tano.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking