Saterdag, Desember 09, 2017

Chama cha mapinduzi wilayani ludewa mkoani njombe kimesema Hakitakuwa tayari kuona kiongozi yoyote anakwamisha ama kubeza shughuli mbalimbali

LUDEWA,
 za kimaendeleo zinazofanyika katika jamii ya wanaludewa.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha mkwimbili kilichopo katika kata ya Lupingu Katibu wa chama  hicho Bakari Mfaume amesema kuwa wao kama chama tawala awatakuwa tayari kuona kiongozi anabeza shughuri za kimaendeleo zinazofanywa na wananchi sambamba  na kuwabeza wananchi ambao wamejitokeza kushiriki katika shughuri hizo.



Kwaupande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya ludewa ambaye pia ni diwani wa kata ya Ibumi Mh Edwadi Haule amewapongeza wananchi wa kijiji hicho kwa kushiri katika shughuli ya uchimbaji wa barabara ya kutoka Ludewa kuelekea Mkwimbili huku akifafanua kwamba wao kamaserikali wanazifahamu changamoto za mkwimbili hivyo wapo tayari kukabiliana na changamoto hizo.

HAULE amewaeleza wananchi hao kwamba swala la kupata mtambo wa kuchimba barabara {PRODOZA }ni gumu na linaitaji uvumilivu huku akielezea kwamba kwa mtambo {PRODOZA} ambao upo kwasasa  unaitajika kuludishwa tarehe 12 mwezi huu huku jitihada za kuomba kuongezewa mda wa kuutumia mtambo huo zikiendelea.

Aidha wananchi wa kijiji cha Mkwimbili wameipongeza halmashauri ya wilayani ya ludewa  kwa kuwapelekea mtambo huo ambao unawasaidia kuijenga barabara hiyo sambamba na kuiomba halmashauri kuwaongezea watumishi wa zahanati ya mkwimbili kwani inawatumishi wachache ambao awakidhi idadi ya watu iliyopo kijijini hapo.

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking