Saterdag, Desember 09, 2017

______________________________________________________

LUDEWA

Wazazi na walezi wa wanafunzi waliohitimi elimu ya msingi hapa nchini
wameshauriwa kuwapeleka watoto wao katika kituo cha Ludewa Education Centre ili waweze kujengewa msingi imara wa maisha yao na uwezo mkubwa wa kitaaluma.

Akizungumza na wazazi wa wanafunzi waliokuwa wakisoma shule ya Ludewa Education Centre Meneja wa Redio Best fm Bw,Nickson Mahundi akiwa mgeni Rasmi kwenye Mahafari ya kwanza yaliyofanyika hii leo katika ukumbi wa CCM amewaasa wazazi na walezi wawapeleke watoto wao katika shule hiyo kutokana na utoaji elimu kutoka kwa walimu wa shule hiyo.

Bw,Mahundi amewapongeza walimu na viongozi wa Ludewa Education Centre kwa jitihada zao hasa kukaa na kuweka mipango mikakati ya kuhakikisha taaluma inakuwa ya kuridhisha shuleni hapo huku akiwapongeza wanafunzi kwa kile walichokipata kwa muda wa miezi zaidi ya Minne.

Agata O.Luoga ni mwanafunzi aliyehitimu elimu ya msingi mwaka huu katika shule ya msingi Mholo iliyopo kata ya Luana ameonyesha kuwa mshindi wa kwanza kwa kila masomo yanayofundishwa hapo kwa kupata alama zaidi ya tisini kwa kila somo alipoulizwa na wanahabari alisema siri kubwa ya yeye kufanya vizuri katika masomo yake ni kuwasikiliza wali wanapowafundisha na kumtanguliza mungu.

Kwa upande wake Bw,Augustino Mwinuka ambaye ni Mkurugenzi wa shule ya Ludewa Education Centre na Nicopolis Accademy mbele ya umati wa wazazi amemwagiza mama mzazi wa mtoto Agata Luoga kumpeleka shule za watu binafsi kutokana na uwezo mkubwa alionao mtoto huyo.

Ikumbukwe kuwa mahafari hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wilayani Ludewa,Wajumbe wa bodi ya shule hiyo,pamoja na wadau mbalimbali wa elimu.

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking