Sondag, Junie 10, 2018

Trump akataa kutia saini tamko la pamoja mkutano wa G7


Mkutano wa kilele wa nchi zenye utajiri wa viwanda G7 umemalizika kwa hali ya  kitisho kipya cha vita vya kibiashara Jumamosi(09.06.2018)wakati rais Trump ghafla alipokataa kutia saini taarifa ya pamoja.

Rais Trump wa Marekani  alimshambulia  kwa  kumtusi  vibaya mwenyeji  wa mkutano  huo  waziri  mkuu  wa  Canada justin Trudeau.

Dakika  chache  baada  ya  taarifa  ya  pamoja  ambayo iliidhinishwa na  viongozi wa  kundi la  washirika  saba kuchapishwa katika  mji  wa  Canada  wa  Quebec  ambao ulikuwa  mwenyeji  wa mkutano  huo, Trump  alianzisha  mashambulizi  katika  ukurasa  wa Twitter kutoka   nje  ya  nchi  hiyo  akiwa  katika  ndege  ya  rais  wa Marekani  ya  Air Force One.

Kiongozi  huyo  wa  Marekani aliondoka  mapema  kutoka  katika mkutano  huo  akiwa  njiani  kwenda Singapore katika  mkutano  wa kihistoria  wa  kinyuklia  pamoja  na  kiongozi wa  Korea  kaskazini Kim Jong Un , na  kuchukua  hatua  ya kutofautiana  na  matamshi ya  waziri  mkuu  wa  Canada  Justin Trudeau  katika  mkutano  na waandishi  habari  kabla  ya  kuondoka nchini  Canada.

"Kwa msingi  wa  matamshi yasiyo  sahihi  ya  Justin  katika mkutano  na  waandishi  habari , pamoja  na  ukweli  kwamba Canada  inatoza  ushuru  mkubwa  kwa  wakulima  wetu , wafanyakazi  na  makampuni  nchini  Marekani, nimewaagiza wawakilishi  wetu  wa  Marekani  kutoidhinisha  tamko  hilo  la pamoja  kwa  kuwa  tunaangalia  kuhusu  ushuru  katika  magari ukisababisha  kufurika  kwa  magari  katika  soko  la  Marekani!. Trump  aliandika  katika  ukurasa  wa  Twitter.

"Waziri  mkuu  Justin Trudeau  wa  Canada  ameonekana  kuwa msikivu na  mtulivu  wakati tulipokutana  katika  mkutano  wa  G7 lakini  alibadilika  na  kutoa  matamshi  katika  mkutano  na waandishi  habari  baada  ya  mimi  kuondoka kwamba .. hatakubali kuburuzwa.' ni uongo na  dhaifu."

Wacaanda ni wapole lakini hawataburuzwa
Hapo  mapema  Trudeau  aliwaambia  waandishi  habari  kwamba uamuzi  wa  Trump  kuweka  usalama  wa  taifa  kuhalalisha  ushuru wa  Marekani  dhidi  ya  bidhaa  zinazoingizwa  nchini  humo  za chuma  cha  pua na  bati , "ni  aina  ya  tusi" kwa  wanajeshi  wa zamani  wa  Canada  ambao  walisimama  pamoja  na  washirika wao  wa  Marekani  katika  mizozo ambayo  ni  pamoja  na  vita vikuu  vya  kwanza  vya  dunia.

"Wacanada  ni  wapole  na waelewa  lakini  pia  hatutakubali kuburuzwa,"  alisema.

Na alisema  amemwambia  Trump "itakuwa kwa  masikitiko  makubwa lakini  itakuwa  kwa  uwazi  kabisa  na  uthabiti  kwamba  tunasonga mbele  na  hatua  za  kulipiza  kisasi  ifikapo  Julai  mosi, kwa kuweka  ushuru  sawa  na  ule  ambao  Wamarekani  wamehalalisha kwa  kutuwekea."



mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking