Donderdag, Februarie 08, 2018

Jaji Mkuu Aionya Serikali



Jaji Mkuu nchini Kenya David Maraga, ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi hiyo katika kukabiliana na upinzani.

 Jaji Maraga ametoa kauli hiyo ikiwa imepita masaa kadhaa tokea kufukuzwa kwa mwanasheria maarufu ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia kuapishwa Raila Odinga katika uwanja wa ‘Uhuru Park’ kufukuzwa nchini humo na kupelekwa Canada.

Katika ukurasa wake wa Twitter Jaji Maraga amesema malalamiko yaliyopelekwa Mahakamani yalikuwa wazi na majukumu ya kufanyia maamuzi yalikuwa ya Mahakama kutokana na kwamba ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe.

Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya Kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama

View image on TwitterView image on Twitter
Please see my Statement on failure to comply with court orders.
Chrispiny kalinga blog

WAFANYAKAZI NJOMBE WAUZWA KUSIKO JULIKANA


KIBENA

Wafanyakazi wa kiwanda  cha chai cha kibena wilayani Njombe Mjini katika Mkoa wa Njombe wanaulalamikia Uongozi wa Kiwanda hicho kwa madai hawatendewi haki stahiki zinazo takiwa kutendewa kwa mujibu wa sheria za kazi.


katika barabara ielekeayo makambako na hapa ni barabarani  kwenye kibao cha kuelekea kwenye kiwanda cha chai kiitwacho kibena tea ltd

Woensdag, Februarie 07, 2018

USHIRIKINA WAINGIA SHULENI LUDEWA, WATOTO WAPELEKWA SHAMBANI



Mwandishi wetu Ludewa

Tatizo la kuanguka mara kwa mara kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muholo iliyopo katika Kijiji cha Muholo kata ya Luana Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Iimeilazimu kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Ludewa Ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ambae ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere Kufika katika Kijiji Hicho ili Kubaini Tatizo.

Bei mpya ya mafuta ya Petroli itakayoanza kutumika leo Februari 7, 2018 kote nchini

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta zinazoanza kutumika leo Februari 7, 2018 huku bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa zikipanda.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzinyangwa Mchany imesema bei za rejareja zimeongezeka kwa petroli ikiwa ni Sh59 sawa na asilimia 2.70, dizeli Sh46 (sawa na asilimia 2.30), na mafuta ya taa kwa Sh24 (sawa na asilimia 1.17).

Amesema bei za jumla nazo zimeongezeka ambazo kwa petroli ni Sh58.57 sawa na asilimia 2.85, dizeli kwa Sh46.48 (sawa na asilimia 2.44) na mafuta ya taa kwa Sh23.75 (sawa na asilimia 1.24).

Mchany amesema ongezeko hilo linatokana na bei kuongezeka katika soko la dunia.

“Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia Bandari ya Tanga nazo zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la Januari 3. Bei za mafuta ya taa hazijabadilika kwa sababu hakuna yaliyoingizwa nchini kupitia bandari hiyo Januari,” amesema Mchany.

Amesema bei za rejareja katika mikoa ya Kaskazini zimeongezeka, ambazo petroli ni kwa Sh15 sawa na asilimia 0.70 na dizeli kwa Sh47 sawa na asilimia 2.29. Bei za jumla zimeongezeka petroli ikiwa ni kwa Sh15.36 sawa na asilimia 0.73 na dizeli Sh47.18 sawa na asilimia2.42.

“Ongezeko la bei za mafuta ya petroli na dizeli katika Mkoa wa Tanga linatokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji,” amesema Mchany.

Kaimu mkurugenzi mkuu huyo amesema sehemu ya shehena kubwa ya mafuta yaliyopokewa katika Bandari ya Dar es Salaam ni yenye bei ya soko la dunia za Novemba, 2017 wakati iliyopokewa katika Bandari ya Tanga ni ya bei ya soko la dunia ya Desemba 2017.

Amesema bei za mafuta katika soko la dunia kwa Novemba 2017 ziko juu kwa zaidi ya asilimia sita ikilinganishwa na bei za Oktoba 2017, wakati bei za Desemba zina mabadiliko tofauti.

Amesema bei ya petroli imepungua kwa asilimia 0.2 na ya dizeli na mafuta ya taa imeongezeka kwa asilimia 2.7 na asilimia 1.9.

“Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ili mradi tu bei hizo zisivuke  bei kikomo kama ilivyokokotolewa na kanuni iliyopitishwa na Ewura,” amesema Mchany



Chrispiny kalinga blog

Hatua utakazotakiwa kuzifuata ili kupata 'passport' mpya ya kielektroniki

Tarehe 31 Januari, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli alizindua mfumo wa uhamiaji mtandao (e-Immigration) ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, kudhibiti ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa raia wa Tanzania na wageni wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali.

Askari Magereza 11 wasimamishwa Kazi

Jeshi la Magereza Tanzania limewasimamisha kazi askari wake kumi na moja waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya mwanakijiji, Aloyce Makalla (41) wiki iliyopita.

Lipumba kufukuza Madiwani Wote wa CUF Dar es Salaam

Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF kwa upande wa Maalim Seif, Mbarala Maharagande amefunguka na kuweka wazi kuwa Profesa Lipumba pamoja na genge lake wamepanga njama kuwafukuza madiwani wote wa CUF Dar es Salaam.

Prof. Jay azuiliwa kumuona Sugu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Nyasa kimedai kuwa mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof. Jay na mkewe wamezuiliwa kuwanona Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga katika Gereza la Ruanda ambako wamewekwa mahabusu.

Tanzania Kinara Utawala Bora Afrika Mashariki....Pia imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika.


Na. Immaculate Makilika

Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani (2017 Democracy Index) iliyozinduliwa Februari 2,  mwaka huu  na kuchapishwa na  jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist  imeitaja  Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika maswala ya Utawala Bora kwenye  ukanda wa Afrika Mashariki.

Serikali yatangaza kuboresha mishahara


Na Chrispin kalinga

Serikali ya Tanzania imeahidi kuanza kuboresha maslahi ya watumishi ya walimu ikiwemo mishahara yao kipindi hiki kutokana na kumaliza zoezi la muda mfupi la uhakiki wa wafanyakazi hewa katika sehemu mbalimbali za ajira.

Msigwa ampa makavu Kigwangala Bungeni

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe. Peter Msigwa amefunguka na kumchana Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala na kudai kuwa anafanya kazi kwa mizuka na mihemko na kuisumbua sekta ya Utalii na Maliasili nchini.

MAHINDI YAUZWA SHILINGI 4800-3500 MKOANI NJOMBE

NJOMBE
Tokeo la picha la mahindiTokeo la picha la mahindi
Tokeo la picha la mahindi

Na  Chrispin kalinga

Wakazi wa Wilaya Njombe Mjini wailalamikia Serikali kwa kuchelewesha kufungua mipaka ya uuzwaji wa zao la Mahindi huku wengine wakisema kuwa wamecheleweshea kutafutiwa Soko la kuuzia mahindi hayo.