Dinsdag, Februarie 27, 2018

Saudi Arabia yawafuta kazi Wakuu wa majeshi

Saudi Arabia imewafuta makamanda wa vyeo vya juu jeshini akiwemo mkuu wa majeshi.

Mfalme Salman pia amefanya mabadiliko kwa makanda wa vikosi vya nchi kavu na vile vya angani.

Taarifa hizo zilichapishwa na shirika rasmi la habari la Saudi Arabia la SPA, lakini hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kwa makamanda hao.

Vanessa Mdee atoa fursa kwa wasicha


Msanii wa muziki Bongo, Vanessa Mdee ametoa mchongo kwa wasichana,Muimbaji huyo wa ngoma Kisela kwa sasa ametangaza kutafuta madansa wa kike

TFF yabadili tena ratiba za Simba na Yanga

Shirikisho la soka nchini limebadili tena ratiba ya ligi kuu soka Tanzania Bara mara hii ikihusisha michezo ya timu za Simba na Yanga kusogezwa mbele na mwingine kurudisha nyuma.

Kwa upande wa mchezo wa Simba SC dhidi ya Stand United uliotakiwa kuchezwa jumapili ya Februari 4, umerudishwa nyuma kwa siku mbili hadi Ijumaa Februari 2, ukipigwa katika uwanja wa taifa Dar es salaam.

Mchezo huo umerudishwa nyuma ili kuipa nafasi klabu ya Simba kujiandaa na mchezo wake wa hatua ya kwanza kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya Misri utakaopigwa Februari 7.

Kwa upande wa Yanga mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa uchezwe Februari 3 kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro umepelekwa mbele na tarehe yake itatajwa hapo baadae.

Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 45 kwenye mechi 19, huku wapinzani wao Yanga wakiwa katika nafasi ya pili na alama 37 kwenye michezo 18. Yanga kesho itakuwa ugenini kucheza na Ndanda FC kwenye mchezo wa ligi kuu.

Chrispiny kalinga blog

Hawa ndio waamuzi watakaochezesha mechi ya Yanga vs Rollers


Shirikisho la mpira wa miguu Africa (CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuwa ndio watachezesha mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi 6, 2018 kwenye uwanja wa Taifa saa 10:30 jioni.

Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland Mangaluso Jabulani Langwenya

Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17, 2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.

Mwamuzi wa kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili Hicham Ait Abou, mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo anatoka Afrika Kusini Gay Makoena.
Chrispiny kalinga blog

Mbowe na wenzake waachiwa kwa dhamana

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wachama hicho wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa Kituo Kikuu cha Polisi tangu saa 6:50 mchana

Diamond Akabidhiwa Rasmi Leseni ya Wasafi TV na Wasafi Redio

Hatimaye Bosi wa Wasafi Classic Baby (WCB) Diamond Platinumz amepata leseni ya kuziweka hewani redio na televisheni za Wasafi zilizobatizwa jina la ‘Wasafi Radio na Wasafi TV’.

Freeman Mbowe na vigogo wengine wa Chadema waripoti polisi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wamekwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi.

DPP akata rufaa hati ya kuzuia dhamana kukataliwa

Mkurugenzi wa Mashtaka DPP amekata rufaa kupinga uamuzi wa Jaji wa Mahakama Kuu, Firmin Matogoro wa kukataa hati ya kuzuia dhamana ya washtakiwa Antonia Zakaria na Timoth Kilumile wanaokabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi.

Mahakama Yaitupa Kesi Ya Mchungaji Mwingira

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na Dk William Morris, raia wa Marekani dhidi ya mkewe Dk Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira.

Watu wawili watiwa mbaroni kwa kuhusika na mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Kinondoni

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Slaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya aliyekuwa Kiongozi wa chama cha Chadema Kata ya Hananasifu, Marehemu Daniel John.

MamboSasa: Ole Wenu Mtakao Andamana....Kitakachotokea Tusilaumiane

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema ni marufuku kwa mwanachi yoyote kushiriki kwenye maandamano kwani hawapo tayari kuona watu wakiandamana na kusababisa uvunjifu wa amani iliyopo.

Tundu Lissu Afunguka Mambo 6 Kuhusu Kifungo cha Sugu

Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu amefunguka kuhusu adhabu ya kifungo cha miezi mitano kwa Mbunge wa Mbeya Mjini na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga.

Sondag, Februarie 25, 2018

Rais Magufuli Ashiriki Ibada Ya Misa Takatifu Iliyofanyika Katika Kanisa La Kigango Cha Mlimani Chato

Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akishiriki Ibada ya misa Takatifu katika kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani)lililopo Wilayani Chato Geita.Februari 25,2018.