Donderdag, Maart 01, 2018

Bao la Kessy latia fola


Bao alilofunga beki wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy limekuwa gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka hasa wale wa mitandaoni katika magrupu mbalimbali.

Mlipuko katika Mahakama ya Kisutu sababu hii


Dar es Salaam.  Shughuli katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zilisimama kwa muda baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme katika transfoma ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) iliyopo katika eneo la mahakama hiyo.

Kikosi maalum kimeundwa na Jeshi la Polisi Pwani


Jeshi la polisi mkoani Pwani limeanzisha kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kufuatilia madereva wanao washawishi askari kupokea rushwa pindi wanapokutwa na makosa mbalimbali ya usalama barabarani.

Tanzania yazikataa meli za Korea Kaskazini

Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Augustine Mahiga amewafahamisha  mabalozi wa nchi tano ambazo ni wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba meli mbili zilizoonekana zikielekea Korea ya Kaskazini zikipeperusha bendera ya Tanzania; zilishafutiwa usajili miaka miwili iliyopita.

Wimbo wa Kibamia wamponza Roma Mkatoliki, afungiwa miezi sita

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amemfungia msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na tasnia ya muziki kwa kipindi cha miezi sita.

Shilole ahukumiwa kulipa faini Milioni 14

Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam imemhukumu msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohamed maarufu Shilole kulipa faini ya kiasi cha shilingi milioni 14, baada ya kupatikana na hatia ya kutapeli na kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye tamasha.

Sh1.9bilioni zatolewa kubotesha vituo vya afya

Serikali  imepeleka Sh1.92bilioni  katika Halmashauri ya mji wa Nanyamba wilayani Mtwara kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya.

Hotuba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali VENANCE MABEYO kat...

HUTUBA YA KAMANDA HII HAPA 


 Chrispiny kalinga blog

Mkuu wa Majeshi: Kuna Viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi, Hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewataka Watanzania kujiepusha na vitendo vinavyoweza kutishia usalama wa nchi na kuharibu tunu ya amani iliyopo.

NEC Yatumiia Hoja 6 Kumzima Mbowe

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesisitiza kuwa itaendelea kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili na taratibu mbalimbali katika kuendesha chaguzi nchini.

BASATA WASHUGHULIKIWE NA ANCO MAGU




Tokeo la picha la basata tanzania
Wanamziki chipkizi Mkoani Njombe wayalauma Mamlaka ya basata kwa kufungia nyimbo za wasanii wa mziki wa kisasa kama ambavyo hivi kalibuni wamefungia nyimbo

Kamati ya Olimpiki yaiondolea adhabu Urusi

Adhabu hiyo ilianza mwezi Disemba mwaka jana
Kamati ya kimataifa ya Olimpiki imeondoa kwenye kifungo Urusi.
Katika taarifa yake imesema adhabu ya Urusi imeondolewa mara moja kuanzia sasa.

Mwalimu aliyefundisha darasa la kompyuta kwa njia ya Ubao azawadiwa

Mwalimu kutoka Ghana alivuma mtandaoni baada ya kuweka picha akichora programu ya Microsoft Word kwenye ubao wakati wa darasa la tarakilishi.

Baada ya picha yake Owura Kwadwo kusambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, kampuni ya Microsoft ilivutiwa na mwalimu huyo na kumsifia kwa jitahada zake za kuwafundisha wanafunzi wake.
Mmoja ya tweet ikisema "Darasa la teknohama Ghana. Hamna Kompyuta? Hamna Shida."
Kujitoa kwake kwa dhati kuliwavutia sana wafanyakazi wa Microsoft, waliandika kwenye akaunti yao ya Twitter, kuwa Bw. Kwadwo atapewa msaada wa vifaa vya kumsaidia katika kazi yake.