Dinsdag, Maart 06, 2018

Manispaa ya Kinondoni Kuboresha Mambo saba

Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo wamefanya mkutano wa Baraza la Madiwani ambapo wamepitia makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida wa mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019.

Magoli ya Township Rollers vs Yanga yaliothibitisha ubora wa Township



Mashabiki wa yanga washika moyo konde



 Chrispiny kalinga blog

Gazeti Lapewa Onyo Kisa Picha za Mange Kimambi

Serikali imetoa onyo kwa gazeti la Tanzanite kwa kosa la kuchapisha picha za utupu.

Gazeti hilo la wiki, limechapisha picha ambazo ni kinyume cha maadili za mwanadada maarufu, Mange Kimambi.

Lema Amjibu Hussein Bashe......"Ni kweli tunahitaji kamati teule kuhusu utekaji ?"

Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amesema kwasasa wanapita katika maumivu makali katika siasa wanazozifanya hivyo hawahitaji kuona sinema tena zikiendelea miongoni mwa wabunge wenzao.

Saba Watiwa Mbaroni Mbeya Kwa Mauaji ya Mlinzi Wa SUMA-JKT

Jeshi  la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia watu saba kwa matukio mbalimbali ya uhalifu, wakiwamo vijana watano wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mlinzi wa SUMA-JKT.

Wanadaiwa kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kumpora bunduki na kutokomea nayo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga, alisema Februari 26, mwaka huu ya saa 1:30 jioni, vijana hao wakiwa na mapanga, walimvamia na kumshambulia mlinzi huyo, Chewe Wilson (34), akilinda kituo cha mafuta cha Manyanya kilichopo Uyole.

Aliwataja vijana hao ni Hamis Shaban (19) na Ibrahim Mbilinyi (22) wote wakazi wa Itezi, Stan Wema (21) mkazi wa Uyole, Bahati Laulend (22) mkazi wa Iduda na Sambaa Samson (32) mkazi wa Isyeseye.

Alisema vijana hao baada ya kumjeruhi wakidhani amekufa walimpora bunduki aina ya Shortgun, mali ya SUMA-JKT aliyokuwa anaitumia na kutokomea nayo.

Hata hivyo, alisema mlinzi huyo alikutwa na wasamaria wema akiwa hai na kukimbizwa katika Hospitali ya Kanda ya Rufani ya Mbeya, lakini akafariki kesho yake kutokana na kuvuja damu nyingi.

“Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata vijana hao na baada ya kupekuliwa walikutwa na bunduki hiyo waliyopora yenye namba za usajili 009009906-MP-18EM-M wakiwa wameificha nyumbani,” alisema Mpinga na kuongeza:

“Vilevile vijana hao wanaojiita ‘Doshaz’ walikutwa na mapanga matatu ambayo mojawapo lilitumika kumjeruhi Chewe na maganda matatu matupu ya risasi, tulipowahoji walikiri kuhusika na tukio hilo na tunatarajia kuwafikisha mahakamani upelelezi ukikamilika.”

Aliongeza kuwa vijana hao walieleza kuna mtu aliwatuma ili wakaibe bunduki hiyo kwa ahadi ya kupewa zawadi ya Sh. milioni tatu.

Katika tukio lingine, watu wawili akiwamo mzee wa miaka 60, wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kosa la kutengeneza bunduki ya kienyeji aina ya Shortgun pamoja na kukutwa na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengenezea silaha hiyo.

Mpinga aliwataja ni Mzee Fadhili Mayenga (60) na Mashaka Samuel (38), wote wakazi wa Kijiji cha Kambikatoto Wilaya ya Chunya.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa Machi Jumamosi mchana kufuatia msako mkali uliofanyika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Kwa mujibu wa Mpinga, baada ya kukamatwa walipekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengeneza silaha hiyo pamoja na risasi 25 za kienyeji ambazo hutumika kwenye silaha hiyo.

Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani muda wowote upelelezi utakapokuwa umekamilika.


Chrispiny kalinga blog

Zaidi ya Vibanda 600 vimeungua katika Ajali ya moto Mbagala

Soko la Kampochea lililopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam limeteketea kwa moto alfajiri ya leo Jumanne Machi 6, 2018 na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.

Sondag, Maart 04, 2018

njombe mji yaitesa ruvushuting

Chrispiny kalinga blog

ASLAY - ANGEKUONA (OFFICIAL VIDEO)


































Chrispiny kalinga blog

Kocha Julio: Yanga sio mbovu kama wengi wanavyodhania

Kikosi cha timu ya Yanga.

KOCHA mwenye mapenzi ya dhati kwa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ametamka kwamba Yanga sio timu mbovu kama wengi wanavyodhani.

Chirwa, Kamusoko waingia Kambini


NYOTA wa Yanga, Obrey Chirwa na Thabani Kamusoko wakiwa na wachezaji wenzao juzi Ijumaa waliingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Breaking News: Watano wapoteza maisha baada ya Hiace ya gongana na Basi la New Force




WATU watano wamepoteza maisha leo asubuhi baada ya basi la New Force lilikokuwa linatokea Msamvu kwenda Mikese kugongana na gari dogo la abiria (Hiace) lililokuwa linatokea Msamvu, mkoani Mogororo.  Pia watu kadhaa ambao idadi yao bado haijajulikana, wamejeruhiwa.

Davido adondoka jukwaani wakati akipanda kwa Mbwembwe


Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido amejikuta akipoteza mzuka baada ya kujikwaa wakati akipanda kwa mbwembwe jukwaani tayari kwa kutumbuiza nchini Rwanda.

Mtu mmoja asiyejulikana ajipiga risasi karibu na geti la Ikulu


Usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 04, 2018 mtu mmoja ambaye jina lake halijatambulika hadi sasa amejiua kwa kujipiga risasi nje ya Ikulu ya Marekani mjini Washington.