Wanachama
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli wameandamana kwenye
ofisi za chama hicho wakitaka aliyekuwa Mbunge wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo(CHADEMA), Julius Kalanga aliyejiunga na chama hicho kufuata
utaratibu ikiwemo hatua za uteuzi wa nafasi ya kugombania ubunge.