Dinsdag, Augustus 07, 2018

Kairuki Atema cheche kwa maofisa madini

 


WAZIRI wa Madini, Angellah Kairuki, amesema hatosita kumtumbua mara moja ofisa wa tume ya madini na ofisa migodi atakayethibitika kumiliki hisa kwenye kampuni za madini au kuwa na leseni ya kuchimba madini.

Watoto Wawili Wafariki Dunia Baada ya Nyumba Kuwaka Moto


Watoto wawili wa kike, mmoja wa mika miwili na mwingine wa miezi 6  wamefariki  dunia baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuungua moto. Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Agosti 7 katika katika kijiji cha Rwazi kata ya Kikuku, Kagera.

Mkuu wa Mkoa Ataka Wahamiaji Haramu Wakamatwe Haraka na Kufungwa

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ameiagiza Idara ya Uhamiaji kuanza msako wa kuwakamata wahamiaji haramu waliojificha kwenye mashamba na majumbani.

Matapeli 13 wa ile pesa Itume kwa Namba Hii wafikishwa Mahakamani


Watu 13 wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwemo utakatishaji fedha wa Shilingi Milioni 154.

Wanachama wa CCM Monduli waandamana kumkataa Mbunge aliyetoka CHADEMA ( Julius Kalanga)


Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli wameandamana kwenye ofisi za chama hicho wakitaka aliyekuwa Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Julius Kalanga aliyejiunga na chama hicho kufuata utaratibu ikiwemo hatua za uteuzi wa nafasi ya kugombania ubunge.

Maandag, Augustus 06, 2018

Nanenane ya kisasa


WAZIRI wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba amewataka waandaaji wa maonyesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane kuhakikisha kuanzia mwaka 2019 wanayaandaa katika sura mpya itakayoleta mabadiliko chanya kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili waweze kuzalisha kwa tija.

Mbao na mitego ya wanyama pori vya kamatwa Lindi


Na.Ahmad Mmow,Lindi.

MBAO 75  na mitego miwili  iliyokuwa inatumiwa na majangiri kutegea wanyama pori,kitongoji cha Namapwiya,Kijiji cha Mnyangala, Kata na karafa ya Mipingo,wilaya na mkoa wa Lindi,

Walimu watakiwa kufuata masharti na miongozo iliyowekwa na Serikali


Na. Thabit Madai, Zanzibar.

Walimu wa Skuli binafsi wametakiwa kuhakikisha wanafuata Masharti na miongozo iliyowekwa na serikali  ili kuimarisha  Elimu ya msingi na sekondari na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini.

Jk ataka teknolojia mpya ya Kilimo


Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametaka teknolojia mpya ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi inayooneshwa kipindi cha Maonesho ya maadhimisho ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama Nanenane iwafikie wananchi ili kuwakwamua katika dimbwi la Umasikini.

Diwani Mwingine wa CHADEMA Kahamia CCM

Madiwani wawili wa Chadema na NCCR-Mageuzi  manispaa ya Bukoba wamejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM, Akiwemo meya wa zamani wa manispaa hiyo, Dk Anatory Aman.

Roma na Stamina Waitwa BASATA

Ikiwa ni siku tatu zimepita tangu wasanii wawili wa hip hop nchini Tanzania, Roma Mkatoliki na Stamina

Wawili Wafariki Dunia kwa Kufukiwa na Kifusi

Watu wawili wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi cha udongo wakati wakichimba madini ya dhahabu katika machimbo madogo yaliyoko mtaa wa Buguti Kata ya Turwa wilayani Tarime.

Saterdag, Augustus 04, 2018

MSANII WA HIP HOP "YLEEZ " KUTOKA NJOMBE AJA KWA MUONEKANO MPYA.



Msanii wa muziki wa Bongo Freva alimaalufu kama Hip Hop ajulikanaye kwa jina  YLEEZ amekutana na chombo chetu cha habari na kuzungumzia haswa