Na Nimrod Process#
Mfanyabiashara maarufu nchini Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe mzito uliosomeka kumlenga mwanamitindo Hamisa Mobeto juu ya wakati mguu anaoupitia.
Zari kupitia ukurasa wake wa Instagram amemtaka Hamisa kusonga mbele bila kugeuka nyuma na hana haja ya kujielezea kwa mtu yeyote juu ya jambo lolote kwani hii ni safari ya maisha yake hivyo hakuna anayehitaji kuelewa zaidi yake.