Vrydag, September 07, 2018

RC Njombe atoa jibu nono kwa wananchi

Image result for ole sendeka






Na Nimrod Mgoye.
Wananchi mkoani Njombe wameiomba serikali kuongeza nguvu ya usimamizi kwa wakandarasi wa miundombinu  hususani ya barabara zinazojengwa mkoani NJOMBE yenye thamani ya Zaidi ya bilioni 400  ili kuwezesha miradi hiyo kujengwa kwa kiwango na kukamilika kwa wakati.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wakazi wa kata ya Njombe mjini wanasema awali kabla ya kuanza kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara hususani kipande cha Lusitu-Mawengi kuelekea wilayani Ludewa inayojengwa kwa kiwango cha Zege wanasema awali hali ya usafiri ilikuwa ni ngumu huku gharama za usafirishaji zikiwa juu.
Kwa upande wake katibu wa itikadi siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe ndug. Erasto ngole  wakati akizungumza na waandishi wa habari anasema serikali ya mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na TANROD wanasimamia vema ujenzi wa miundo mbinu hiyo huku akiongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara nne kubwa zitawaunganisha wananjombe na fursa mbali mbali za maendeleo.
Naye mkuu wa mkoa wa Njombe mh.CHRISTOPHER OLESENDEKA anasema serikali ya mkoa wa Njombe itaendelea kusimamia kikamilifu na kukamilisha kwa wakati miradi yake ikiwemo nyumba za serikali.
mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking