Vrydag, Februarie 16, 2018

Babu Seya, Papii Kocha Wawaliza watu.....Tazama Hapa Video Yao Mpya

Msanii wa muziki wa 'Papii Kocha' ambaye alikuwa amefungwa kwa zaidi ya miaka 13 jela leo Februari 16, 2018 ameachia video ya wimbo wake mpya 'Waambie' ambao umewaliza baadhi ya watu kutokana na mambo ambayo ameyaimba ndani ya wimbo huo.

Woensdag, Februarie 14, 2018

MKURUGENZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI ASEMA NENO ZITO MKOANI NJOMBE


Picha na France malekela
wa kwanza kushoto kwako ni mkurungenzi mkuu wa chuo

Yanga yaipiga Majimaji FC 4-1

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC wamefanikiwa kuchomoza na ushindi mujarabu wa mabao 4 – 1 dhidi ya Majimaji FC mchezo uliyopigwa jijini Dar es salaam.

DR Congo: Wanajeshi watano wafariki katika msafara wa rais

Wanajeshi watano wafariki katika ajali iliotokea katika msafara wa rais Joseph Kabila Minkelo Kusini-Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Halmashauri Ya Longido Yapewa Gari La Chanjo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi mbunge wa jimbo la Longido, Dkt. Stephen Kiruswa gari aina Tunland Double cabin kwa ajili ya kuboresha huduma za chanjo na afya katika jimbo hilo.

Mwigulu Nchemba awakemea wanasiasa wanaoihusisha Serikali na kushambuliwa kwa Tundu Lissu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kuumia kwa mbunge Tundu Lissu kama chambo ya kisiasa katika majukwaa.

Waziri Mkuu: Bil. 161.9 Zimetumika Kuboresha Vituo Vya Afya 170

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia sh. bilioni 161.9 kuboresha vituo vya afya 170 nchini pamoja na kugharamia huduma ya Afya ya Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa maisha yao.

Dinsdag, Februarie 13, 2018

Rais Zuma akubali kujiuzulu Lakini kwa Masharti

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekubali kuachia madaraka ya kuongoza nchi hiyo, baada ya wito uliotolewa na chama chakle ANC kumtaka kujiuzulu ndani ya masaa 48.

Sondag, Februarie 11, 2018

UMEME WA BAYOGESI WAINUKA

Bayogesi (biogas) ni kitu gani?
Bayogesi ni mchanganyiko wa gesi inayoundwa na viasilia mbalimbali vinavyotengenezwa katika mazingira ya kutokuwepo hewa (oksijeni) ambayo asilimia kubwa ni gesi ya

Vijiji 100 kupata maji ya Ziwa Victoria


WIZARA ya Maji na Umwagiliaji inatekeleza mradi wa maji wa vijiji 100 vilivyopo kandokando ya bomba kuu kutoka Ziwa Victoria hadi Kahama Shinyanga, Bunge limeelezwa.

Tanzania kujiondoa katika mpango wa kuwasaidia Wakimbizi



Serikali ya Tanzania inasema kuwa inajiondoa katika mpango wa Umoja wa mataifa wa kuwasaidia wakimbizi kuanza maisha mapya katika mataifa yanayowahifadhi.

MAKON DA AZITUMBUA MAHAKAMA ZA KATA

Picha ya David Maphone

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda, leo amesimamisha shughuli za Mahakama za Kata(Mabaraza ya kata) kwa maelezo kwamba hazina Wanasheria wanaojua Sheria inayoweza kutoa haki, RC Makonda anapokea malalamiko ya wananchi wa mkoa wa Dar Es Salaam, katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

TANGA RAHA- Sehemu ya Kwanza (1)









































MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

Ni siku ya utambulisho mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari moja jijini Tanga nikiwa mimi na mwalimu mwenzangu ambaye wa kike ambaye ndio tumetoka chuo cha ualimu na kupangiwa shuleni hapa
Akaanza mwenzangu kujitambulisha ambaye, akapigiwa makofi na wanafunzi kisha nikafwatia mimi kujitambulisha

"Mimi ninaaitwa Sir Eddy nitafundisha Biology na Chemisty"
Wanafunzi wote wakapiga makofi ma vigelegele hukt wakionekana kupendezwa na utambulisho wangu mfupi na wakueleweka.Muda wa masomo nikakabithiwa kuanza na kidato cha nne katika somo la Biology ambao ndio nao wanaanza mwezi wa kwanza wa muhula wa masomo.Nikaanza kuuliza mwanafunzi mmoja mmoja jina lake ili kuniwia rahisi kuwafundisha na kuwazoea kwa haraka
Nikaanza kipindi huku nikiwauliza uliza maswali ya mada walizo zisoma wakiwa kidato cha tabu, ili niweze kwenda nao sawia kwenye kufundishana
"Ulisema unaitwa nani, binti?"
"Rahma"
"Ehee elezea Reproduction(uzalishaji) kwa mwanadamu inakuwa vipi?"
Akanza kuelezea hatua moja baada ya nyingine kuanzia mtoto anavyo tafutwa hadi kuzaliwa bila hata kukosea.Wanafunzi wenzake wakampigia makofi huku wengine wakitaka kutokana na baadhi ya vitu alivyokuwa akivizungumza
Wakanipa ushirikiano mzuri hadi nikamaliza kipindi na kurudi zangu, ofisini nikisubiri kwenda darasa jengine
Muda wa kutoka ukawadia nikabeba begi langu lenye laptop yangu niliyo hifadhi vitu vyangu mbalimbali
"Sir ninaweza kukusaidia kubeba begi?"
"Rahma ndio unaweza kunisaidia"
Rahma yupo na mwenzake ambaye sikumuona darasani wakati nilipokuwa ninafundisha somo langu
"Unakalia wapi?"
"Maeneo sijui wanapaita Chuda, kitu kama hicho"
"Sir Eddy kwani Tanga wewe ni mgeni?"
"Nimgeni nina kama siku ya nne leo, tangu nije bado majina yana nisumbua sumbua kuyashika"

"Umetokea wapi?"
"Arusha"
Tukatembea njia nzima huku tukizungumza mambo mengi, kuhusiana na mji huu ambao nyumba zake zimepangika vizuri kwa mpangilio wa mistari mistari, nitofauti sana na mji kama Dar es Salaam.Tukafika nyumbani kwangu na nikawakaribisha na sote tukaingia ndani kuingia ndani
"Ehe sir Eddy umejitahidi?"
Rahma ni muongeaji sana kiasi kwamba hakuwa anampa mwenzake nafasi, ya kuzungumza na mimi japo hata kuchangia mada ya jambo tunalo lizungumzia
"Nimejitahidi vipi?"
"Chumba chako ni kizuri"
"Asante"
"Sir acha sisi twende tutakuja kukutembelea jumamosi"
"Sawa karibuni"
Wakaondoka na kuniacha nikiendele na shughuli zangu za kawaida, ikiwemo kupika chakula cha mchana, nilicho kijumlisha na chakula cha usiku.Nikaendelea kufanya kazi kwa juhudi siku zote za kazi yangu, huku upendo wangu wa kuipenda kazi yangu ukizidi kuongezeka kadri ya siku zilivyozidi kukatika....

Chrispiny kalinga blog