Maafisa kutoka Mashariki mwa Afghanistan wanaarifu kuwa watu kumi na nne wamekufa na wengine na kadhaa walijeruhiwa katika mlipuko kwenye msikiti katika jimbo la Khost.
Watu sita wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka bahari, karibu na Kisiwa cha Mafia Tanzania,kutokana na dhoruba kali.Mbunge wa jimbo la Mafia, mkoani Pwani Mbaraka Dau amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Rais Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa serikali kuacha kutoza ushuru kwa wananchi wanaosafirisha bidhaa na mazao ambayo hayajafika uzito wa tani moja, kwakuwa bunge mwaka 2017 lilipitisha sheria ya kufuta tozo zaidi ya 87 katika sekta ya kilimo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo, ametekeleza kwa vitendo agizo alilopewa na Rais Magufuli, la kwenda kijijini Tundu, Wilayani Mikumi kushughulikia kero ya mradi wa maji kijijini hapo.
Rais John Magufuli ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Morogoro, kuweka utaratibu mzuri ili wamachinga waweze kuuza bidhaa zao ndani ya stendi ya mabasi ya Msamvu ya mjini Morogoro.
Klabu ya soka ya Yanga imeungana klabu ya soka ya Manchester United na mashabiki wengine wa soka duniani kumuombea apone haraka kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson ambaye amefanyiwa oparesheni ya Ubongo.
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu machinga kujisajili na kupata vitambulisho lengo likiwa kuwatambua katika sekta isiyo rasmi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kwamba watu wanaokula fedha za serikali wanajitafutia balaa, kwani ni sawa na wanakunywa sumu.
Wakazi wa Kijiji cha Matema Wilayani Kyela Mkoani
Mbeya wamezungumza na waandishi wa habari juu ya uwepo wa Ziwa Nyasa na wananufaika vipi kwa uwepo wa ziwa hilo na
huku wengine wakisema kuwa licha ya mafanikio hapakosi changamoto.
Picha na Francis Malekela Baadhi ya wanafunzi walio fanya Ziara ziwa Nyasa.
MBEYA .
NA MWANDISHI WETU
Wanachuo wa Chuo cha Uandishi wa Habari Eckros School of Journalism kilicho Mkoani Njombe wamefanya Ziara ya kimasomo katika Kijiji cha
Matema Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwenye
Ziwa Nyasa kwa lengo la kujifunza kwa vitendo.