Msanii
mkongwe na miongoni mwa waasisi wa muziki wa BongoFleva, Juma Nature
amefunguka na kuwaonya wasanii wa sasa kuacha tabia ya kuigana na
kubweteka katika kufanya kazi zao kwa kuwa kitendo hicho kinapelekea
kuua muziki.
Juma Nature ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha EATV baada ya kuwepo minong'ono mingi kwa mashabiki na wadau wa muziki nchini kulalamikia vitendo vya baadhi ya wasanii kutokuwa wabunifu katika ufanyaji kazi zao
"Hii
ni kazi lakini wengine wanachukulia ubishoo. wasanii wanabweteka sana
na hilo ndio tatizo kubwa la vijana wa sasa hivi akitoa nyimbo moja
anajiona ameshaweza kila kitu. Nawaambia kitu kimoja kwamba wakongwe
tumesharudi na hatuwezi kukubali kuona wanakuja watu wengine kutoka
sehemu zingine watupite tunawaona hivi hivi, mimi sikubali nasema hata
kidogo", amesema Nature.
Pamoja
na hayo, Nature ameendelea kwa kusema "sasa hivi wasanii ni wengi sana
halafu wengi wao wanaigana ndio maana unakuta hakuna ushindani. Nadhani
imefika wakati hawa wasanii wetu kujifunza na kuacha uvivu katika kazi
zao za muziki waufanye kazi ambayo itawasaidia wao pamoja na vizazi vyao
vitakavyokuja".
Kwa
upande mwingine, Juma Nature amesema kilichosababisha wasanii wakongwe
'zamani' ikiwemo yenye mwenyewe ni nyimbo zao kudumu mpaka miaka hii ni
kutokana na maudhui ya kazi kutofanana kwasababu kila mmoja wao alikuwa
mbunifu.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking