Rais
wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa tayari
amemaliza ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku mbili nchini Tanzania,
Rais John Pombe Magufuli ambaye alikuwa mwenyeji wake amemsindikiza
katika viwanja vya ndege vya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere tayari
kurejea nchini kwake.
Ujio
wa Rais huyo umejikita katika mambo matatu ambayo Rais Magufuli
aliyasema pindi alipoongea na waandishi wa habari Ikuli jijini Dar es
salaam, ambapo alisema wamezungumza jinsi ya kuimarisha uchumi wa nchi
hizi mbili kiuchumi tofauti na uhusiano wa zamani uliokuwa wa kisiasa
zaidi.
Pia
wamekubaliana kupitia jumuiya ya Ushirikisho wa Nchi za Kusini mwa
Afrika (Sadc), kukuza biashara ambapo amesema ipo mikataba mbalimbali ya
kulegeza masharti ya kibiashara katika Sadc.
Rais Mafuli ameongezea kuwa wamekubaliana kukuza uwekezaji ambapo watashirikiana kutumia kwa wingi vivuto vilivyopo hapa nchini.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking