Na Mathias Canal-WK, Singida
Waziri
wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Mrakibu wa polisi Wilaya
ya Iramba ASP Magoma Mtani kumkamata aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya
Chama cha ushirika (AMKOS) Msai.
Waziri
Tizeba ametoa agizo hilo jana 9 June 2018 Mara baada ya kutembelea
kitongoji cha Kati, Msai na Mtoa akiwa katika ziara ya kikazi ya Siku
mbili kwa ajili ya kutembelea vituo vya ununuzi wa pamba na kujionea
msimu wa ununuzi wa zao hilo katika vijiji hivyo.
Dkt
Tizeba amelaani vikali ufujaji huo wa fedha za wakulima huku akimtaja
Paul Ramadhan Kurwa kuhusika na ufujaji huo wa shilingi milioni 23 huku
akiendelea kuonekana mtaani pasina kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Wakati
muelekeo wa serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu Dkt John Pombe
Magufuli ukijipambanua kutaka kuboresha maisha ya watanzania kupitia
Kilimo lakini kuna watu wanataka kurudisha nyuma juhudi hizo, hakika
tutawapa kibano kweli kweli hakuna utani kwenye fedha za wananchi"
Alikaririwa Dkt Tizeba
Mhe
Tizeba ametoa siku moja kukamatwa kwa mwizi huyo na kufikishwa
mahakamani ili awe mfano kwa wezi wengine wasio kuwa na haya wala soni.
Aidha,
amewataka wananchi katika msimu huu wa uuzaji na ununuzi wa Pamba
kutouza Pamba zenye uchafu wakidhani wataongeza idadi ya kilo kwani
kufanya hivyo ni kufifihisha juhudi zao wenyewe jambo ambalo halina
tija.
Sambamba
na hayo pia amewaondoa hofu wakulima kote nchini kuwa serikali ya awamu
ya tano inatekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi yenye mkataba na wananchi katika kipindi cha miaka mitano
2015-2020.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula
amempongeza Waziri Tizeba kwa kutembelea maeneo mbalimbali ili kujionea
ununuzi wa Pamba huku akiwasihi wananchi wilayani humo kulima kiasi
kikubwa cha Pamba msimu ujao kwani mbegu na madawa ya kuulia wadudu
vitatolewa bure kuanzia msimu ujao wa mwaka 2018/2019.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking