Saterdag, Junie 30, 2018

Ray C: “Nilikuwa Siwezi Kupanda Stejini Bila Kutumia Madawa Ya Kulevya”


Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amefunguka na kuelezea kipindi kigumu alichopitia wakati ameathirika na madawa ya kulevya.

Ray C ambaye kwa sasa anaishi nchini Kenya na kufanya kazi zake kimuziki amefunguka alipohudhuria kongamano la madawa ya kulevya Mombasa.
 
Ray C alipata  nafasi ya kuongelea kuhusu madawa ya kulevya kutokana na yeye kuwa muhanga mkubwa wa madawa hayo ambapo kwa sasa amekiri kuacha  kutumia madawa.

Ray alifinguka kuwa ilifika kipindi akawa mtumwa wa madawa ya kulevya kiasi ya kwamba alikuwa hawezi kupanda hata stejini kutumbuiza bila kutumia madawa ya kulevya.

"Addiction took three of the best of me. I was heartbroken. My brain was taken away by drug use. 
"My brain was not working because there was something else in my brain telling me I could not perform on stage without drugs, that I could not do anything without drugs. 
"I could not go anywhere without drugs, therefore I was a prisoner in my own soul. 
"Wengi wanaoingia kwenye madawa, watu wanaathirika maini kwenye madawa, watu wanatumia sindano pamoja wanapata HIV, wanawake wanajiuza ili mradi aweze kupata pesa aweze kukidhi ule utegemezi wake”

Tangu Ray C aache kutumia madawa ya kulevya ameonekana kufanya vizuri zaidi na hata kurudi kufanya muziki
mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking