Mshambuliaji
wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez, amesema kwa sasa yupo FIT,
tofauti na alivyoanza michezo ya hatua ya makundi katika fainali za
kombe la dunia, zinazoendelea nchini Urusi.
Suarez
ameweka wazi utimamu wake wa mwili, akiwa katika mkutano na waandishi
wa habari uliokua unazungumzia mpambano wa leo wa hatua ya 16, ambao
utawakutanisha na mabingwa wa soka barani Ulaya Ureno.
Mshambuliaji
huyo wa klabu ya Barcelona ya Hispania, amesema katika michezo ya hatua
ya makundi hakuwa katika kiwango kizuri japo alibahatika kufunga bao
walipocheza dhidi ya wenyeji Urusi, lakini kwa siku kadhaa alizofanya
mazoezi kwa ajili ya mchezo wa hii leo, anajihisi yupo katika kiwango
bora.
“Nipo
vizuri tofauti na nilivyokua mwanzo, nimejaribu kufanya mazoezi kwa
kiwango kikubwa na nimefanikiwa, ninajihisi tofauti na ilivyokua katika
mchezo wa kwanza dhidi ya Misri na kisha Urusi.
“Binafsi
nilikua najitafakari mara baada ya michezo niliyocheza, nilifahamu
sikucheza vizuri, nilitumia majibu ya maswali niliyokua najiuliza
kufanya mazoezi katika kiwango cha hali ya juu, hadi ninazungumza nanyi,
ninaamini kesho (leo) nitacheza vizuri sana.
“Kwa
upande wa timu, kiujumla tupo tayari kwa mpambano dhidi Ureno,
tutahakikisha tunacheza kwa ushirikiano wakati wote, ili tufanikishe
lengo la ushindi na kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.”
Uruguay
ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi la kwanza
lililokua na wenyeji Urusi, Misri na Saudi Arabia, kwa kufikisha alama
9.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking