Mkutano wa kilele wa nchi zenye utajiri wa viwanda G7 umemalizika kwa hali ya kitisho kipya cha vita vya kibiashara Jumamosi(09.06.2018)wakati rais Trump ghafla alipokataa kutia saini taarifa ya pamoja.
Rais Trump wa Marekani alimshambulia kwa kumtusi vibaya mwenyeji wa mkutano huo waziri mkuu wa Canada justin Trudeau.
Dakika chache baada ya taarifa ya pamoja ambayo iliidhinishwa na viongozi wa kundi la washirika saba kuchapishwa katika mji wa Canada wa Quebec ambao ulikuwa mwenyeji wa mkutano huo, Trump alianzisha mashambulizi katika ukurasa wa Twitter kutoka nje ya nchi hiyo akiwa katika ndege ya rais wa Marekani ya Air Force One.
Kiongozi huyo wa Marekani aliondoka mapema kutoka katika mkutano huo akiwa njiani kwenda Singapore katika mkutano wa kihistoria wa kinyuklia pamoja na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un , na kuchukua hatua ya kutofautiana na matamshi ya waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau katika mkutano na waandishi habari kabla ya kuondoka nchini Canada.
"Kwa msingi wa matamshi yasiyo sahihi ya Justin katika mkutano na waandishi habari , pamoja na ukweli kwamba Canada inatoza ushuru mkubwa kwa wakulima wetu , wafanyakazi na makampuni nchini Marekani, nimewaagiza wawakilishi wetu wa Marekani kutoidhinisha tamko hilo la pamoja kwa kuwa tunaangalia kuhusu ushuru katika magari ukisababisha kufurika kwa magari katika soko la Marekani!. Trump aliandika katika ukurasa wa Twitter.
"Waziri mkuu Justin Trudeau wa Canada ameonekana kuwa msikivu na mtulivu wakati tulipokutana katika mkutano wa G7 lakini alibadilika na kutoa matamshi katika mkutano na waandishi habari baada ya mimi kuondoka kwamba .. hatakubali kuburuzwa.' ni uongo na dhaifu."
Wacaanda ni wapole lakini hawataburuzwa
Hapo mapema Trudeau aliwaambia waandishi habari kwamba uamuzi wa Trump kuweka usalama wa taifa kuhalalisha ushuru wa Marekani dhidi ya bidhaa zinazoingizwa nchini humo za chuma cha pua na bati , "ni aina ya tusi" kwa wanajeshi wa zamani wa Canada ambao walisimama pamoja na washirika wao wa Marekani katika mizozo ambayo ni pamoja na vita vikuu vya kwanza vya dunia.
"Wacanada ni wapole na waelewa lakini pia hatutakubali kuburuzwa," alisema.
Na alisema amemwambia Trump "itakuwa kwa masikitiko makubwa lakini itakuwa kwa uwazi kabisa na uthabiti kwamba tunasonga mbele na hatua za kulipiza kisasi ifikapo Julai mosi, kwa kuweka ushuru sawa na ule ambao Wamarekani wamehalalisha kwa kutuwekea."
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking