Woensdag, Januarie 31, 2018

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya January 31


chrispiny kalinga

Serikali Yasisitiza Uwazi Shughuli Za Madini


Kampuni za Madini nchini zimetakiwa kufanya shughuli zake kwa uwazi sambamba na kufuata Sheria za nchi ili kuepuka migongano.

Wachimbaji Wanne wafariki kwa kufukiwa na kifusi Arusha


 Wachimbaji wanne wamefariki na  mmoja yupo mahututi baada ya kuangukiwa na Ngema  walipokuwa wakipakiza  changarawe kwenye gari katika machimbo ya changarawe yaliyopo katika mlima Murieti katika jiji la Arusha.

Rais Magufuli Kuzindua Pasipoti ya Kielektroniki


Na Jonas Kamaleki
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli leo  atazindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Familia ya lissu Yahofia Tundu Lissu Kufukuzwa Hospitali



Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), imelitaka Bunge kutoa fedha za matibabu yake kama halitaki mtunga sheria wake huyo akafukuzwe hospitalini alikolazwa.

Raila Odinga hatarini kushtakiwa kwa kujipa urais nchini kenya


MAMLAKA za Kenya, jana zilizima vituo vya televisheni kuzuia matangazo 'live' ya sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, ambaye alisusia uchaguzi wa marudio wa mwaka jana uliobishaniwa.

NECTA Watangaza Matokeo ya Kidato Cha Nne 2017....Bofya Hapa Kuyatazama



Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba.

LUDEWA MKUU WA WILAYA YA LUDEWA MKOANI NJOMBE ATOA KAULI NZITO JUU YA YEYOTE ATAKAYE KUTWA AMESIMAMA NA WANAFUNZI.





 Na chrispiny kalinga.

wananchi wilayani ludewa mkoani njombe katika kata ya mlingali na wanaulalamikia uongozi wa shule za sekondari zilizopo katika kata hizo kwa madai ya kutozwa chakula cha watoto wao kisicho pungua debe kumi ambazo ni sawa na kilo mia moja.

LUDEWA WALIMU WA SHULE YA MSINGI WAWAAMURU WANAFUNZI KWENDA KULIMA SHAMBA LA MWALIMU MUDA WA MASOMO.



 
Na chrispin kalinga. 
 
Walimu wilayani ludewa mkoani njombe katika kata ya lubonde shule ya msingi masimbwe wawaamrisha wanafunzi kwenda kulima shamba la mwalimu wa awali muda wa masoma.

Dinsdag, Januarie 30, 2018

SIKU 14 ZA DANGOTE VIONGOZI WAKAZA KAMBA KUMTAZAMA



Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa siku 14 kwa uongozi wa kiwanda cha saruji cha Dangonte mkoa wa Mtwara kuingia mkataba na wachimbaji wadogo wa gypsum.
Biteko ametoa kauli hiyo leo Januari 21, 2018 baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza na viongozi wake.


MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKAGUA STENDI MPYA NA SOKO NJOMBE,


Mkuu wa Mkoa Wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Akitoa maagizo Kwa wataalamu wa Ujenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Akiwa Katika Stendi mpya Njombe Mjini. 
Kulia ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Bw,Erasto Ngole Akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Katika Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Stendi mpya ya Magari Njombe mjini. 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Akitembelea na Kukagua maeneo mbalimbali Ndani ya Stendi Mpya ya Njombe, Mjimwema. 

Wakwanza Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri Aliyeambatana  na Mkuu wa Mkoa wa Njombe katika Ziara hiyo. 
Nimwonekano wa baadhi ya Maeneo katika Stendi mpya ya Magari Njombe Mjini katika eneo la Mjimwema, 
Jengo la Vyoo na Bafu Katika Stendi Mpya ya Magari Njombe Mjini.

Na Maiko Luoga Njombe,
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Mapema Leo January 23 ,2018 Ametembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi Njombe Mjini Mradi ambao unaendelea kwakusuasua na Mkandarasi hayupo Saiti.

Baada ya kukagua Stendi hiyo ya mabasi Njombe, Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe amebaini Kuwa kuta za Stendi hiyo zimejengwa Chini ya kiwango kwakuwa kabla ya Kuanza kutumika tayari Kuta hizo zimeshatengeneza Nyufa Licha ya Jengo hilo la stendi kutumia pesa nyingi za Serikali hatahivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe amewaagiza Wataalamu wa Ujenzi Kuhakikisha Sehemu zote zenye matatizo zinarekebishwa na Hatua stahiki zakisheria Zinachukuliwa Kwa wote waliosababisha Upungufu huo wa jengo la Stendi mpya ya mabasi Njombe Mjini.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Wa Njombe pia Kwakuambatana na Uongozi wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe akiwemo Katibu wa chama hicho Mkoa wa Njombe Bw. Hosea Mpagike na Katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Bw. Erasto Ngole kwapamoja wametembelea na kukagua Ujenzi wa Mradi wa Soko Jipya la Wafanyabiashara Mjini Njombe Kisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe alitoa maagizo Kwa Mkurugenzi wa mji wa Njombe Kuhakikisha ujenzi huo unakamilika Kwa haraka ili wafanyabiashara waweze kuendelea na Biashara zao.

Alipowasili Katika eneo la Soko kuu la wafanyabiashara Njombe mjini Mkuu wa Mkoa Hakuwakuta viongozi wa kata ya Njombe mjini na kupewa Maelezo kuwa viongozi hao wapo Katika kikao cha Kata ambapo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Alitoa Amri kuwa Viongozi hao waache kikao chao maramoja na kisha wahudhurie mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe akizungumza na wafanyabiashara Katika soko kuu la wafanyabiashara Njombe Mjini.
Endelea kutembelea www.maikoluoga.blogspot.com Kwa Habari zaidi
chrispiny kalinga

ZAO LA PARETO LAPEWA KIPAUMBELE LUDEWA, SOKO LIKO WAZI NDANI NA NJE YA TANZANIA


Bw,Godfrey Mbeyela Meneja wa PARETO Mkoa wa Njombe akifafanua Ubora Wa PARETO Mbele wa Baraza la madiwani Ludewa.
Bei za PARETO kwa kilo Kulingana na Ubora wake
 Na Maiko Luoga Ludewa,
Wananchi wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe wameshauriwa Kulima mazao yakibiashara Ikiwemo PARETO,KOROSHO, KAHAWA NK, yenye soko la Uhakika ndani na nje ya Tanzania ili kuweza kujikwamua Kiuchumi kutokana na Mazao mengi wanayolima Wakulima Wilayani Humo Ikiwemo mahindi Kukosa Soko Huku wakulima wakiishia Kukaa na mazao yao Ndani ya nyumba Bila kupata Faida.

Ushauri huo ulitolewa na Meneja wa Zao la PARETO Mkoa wa Njombe Bw, Godfrey Mbeyela wakati akifafanua Faida za Zao hilo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Kwa Robo ya Pili ya Mwaka 2017 / 2018 kwakipindi cha Kuanzia Mwezi October hadi December 2017 Mkutano uliofanyika January 27 Mwaka huu 2018 Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.

Meneja huyo Wa PARETO Mkoa wa Njombe aliwaomba Madiwani wote katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kufikisha Ujumbe kwa wananchi katika Maeneo yao ili waweze Kulima kwa wingi Zao hilo la PARETO ambalo linaelezwa kuwa na Faida kubwa zaidi kwa Mkulima Kwakuwa PARETO Inavunwa mara kwa mara iwapo Shambani na Mkulima atauza Mazao yake kisha Kulipwa pesa yake kulingana na Mzigo Aliouza.

Akieleza Bei za Zao La PARETO Mbele ya Madiwani wa Halmashaurui ya Wilaya ya Ludewa Meneja wa Zao hilo Bw, Mbeyela Alisema kuwa kwa Msimu wa Mwaka 2017/2018 Pareto Imekuwa ikiuzwa Kuanzia Tsh, 3300 Hadi 2300 Kwa kilo Moja ya Zao hilo la Patreto huku akiwahakikishia wananchi wa Ludewa kuwa Kampuni inayojishuhgulisha na Zao hilo ndani na Nje ya Tanzania ijulikanayo kwa Jina la PYRETHRUM COMPANY OF TANZANIA LIMITED (PCT) Imejenga Kiwanda katika Eneo la Mafinga Mkoani Iringa Kwaajili ya Kununua PARETO Kwa wakulima watakao zalisha zao hilo.

Hatahivyo Kampuni ya PYRETHRUM COMPANY OF TANZANIA LIMITED (PCT) yenye Soko la PARETO ndani na Nje ya Tanzania Inatoa Miche Bure kwa wakulima wa zao hilo ambao wanahitaji Kulima zao hilo.

Katika Hatua Nyingine Meneja wa PARETO Mkoa wa Njombe  Bw, Godfrey Mbeyela ameweka Bayana Taratibu na Ushauri wa Kuuza PARETO Kiwandani kuwa ni pamoja na Wakulima kuuza PARETO yao moja kwa moja Kiwandani ili kuboresha zaidi mapato yao na Kuongeza kuwa Wakulima wanashauriwa Kujiunga katika Vikundi kuanzia watano na kuendelea pamoja na Kupata kibali au kitambulisho kutoka kwa Uongozi wa Kijiji wanapotoka, juu ya nia yao ya Kuuza Pareto moja kwa Moja Kiwandani Wakiwa na Muhtasari wa Kuanzishwa kwa kikundi chao na Kibali cha Kijiji kisha watafika Kiwandani na Kupata Mkataba Tayari kwakuuza Pareto yao.

Bw, Mbeyela Aliongeza kuwa Wakulima Baada ya Kupewa Mkataba wataelekezwa namna ya Kupata Leseni Kutoka Bodi ya Pareto Tanzania inayowaruhusu kufanya Biashara ya PARETO kisha kijiji kinashauriwa Kutunza Orodha ya Vikundi vyake vyote na nakala itawasilishwa Kiwandani.

Nchini Tanzania Zao la PARETO Linaelezwa kustawi kwa wingi katika Mikoa wa Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania katika Mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa na Kiasi kidogo katika kanda ya Kaskazini Mkoa wa Arusha Pia Kampuni ya PYRETHRUM COMPANY OF TANZANIA LIMITED (PCT) Inamsaidia Mkulima Bora wa Pareto Kujua namna ya kuandaa Shamba la kuzalisha Zao hilo kuwa ni Pamoja na Mkulima Kuchagua eneo lenye Rutuba ya Kutosha, Kusafisha Shamba na Kuondoa magugu yote Shambani, Pamoja na Kulima vizuri shamba la PARETO.

Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh, Edward Haule pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Ya Ludewa Bw, Ng'wilabizu Ndatwa Ludigija, Madiwani pamoja na Watumishi wa Halmasahuri ya Wilaya ya Ludewa Wameipongeza kampuni hiyo ya  PYRETHRUM COMPANY OF TANZANIA LIMITED (PCT) Kwakuamua kulifufua zao la PARETO Katika wilaya ya Ludewa kwakuwa wananchi waliamua kuacha kuzalisha zao hilo kutokana na Ukosefu wa soko hivyo kwasasa Viongozi hao wameuahidi Uongozi wa kampuni hiyo kuwa watawaelimisha wananchi ili waweze kuzalisha zao hilo kwa wingi zaidi.

chrispiny kalinga

Tumia mchanganyiko wa papai na asali kuondoa madoa usoni


KUMEKUWA na sababu mbalimbali zinazofanya watu kutokuwa na ngozi zisizokubalika.Mbali na hali ya hewa pia matumizi ya pombe na sigara hata matumizi ya cream kali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu