Woensdag, Januarie 31, 2018

Shule 10 BORA na Shule 10 za Mwisho Matokeo ya Kidato cha Nne 2017


Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne kwenye mtihani ambao ulifanyika October 2017 ambapo Shule  iliyoshika namba moja inatoka Mbeya.

TOP 10 YA SHULE BORA.

1. St. Francis Girls ya Mbeya

2. Feza Boys ya Dar es salaam

3. Kemebos ya Kagera 

4. Bethel Sabs Girls ya Iringa 

5. Anwarite Girls ya Kilimanjaro 

6. Marian Girls Pwani 

7. Canossa ya Dar es salaam 

8. Feza Girls ya Dar es salaam 

9. Marian Boys ya Pwani 

10. Shamsiye Boys ya Dar es salaam 

TOP 10 YA SHULE ZA MWISHO KITAIFA
10. Mtule ya Kusini Unguja

9. Nyeburu ya Dar es salaam

8. Chokocho ya Kusini Pemba

7. Kabugaro ya Kagera

6. Mbesa ya Ruvuma

5. Furaha ya Dar es salaam

4. Langoni ya Mjini Magharibi

3. Mwenge S.M.Z ya Mjini Magharibi

2. Pwani Mchangani ya Kaskazini Unguja

1. Kusini ya Kusini Unguja

chrispiny kalinga

Umri wa Kustaafu Kwa Madaktari Bingwa, Wahadhiri Waandamizi na Maprofesa Sasa miaka 65


Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswaada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298  (The Public Service Act) itakayowezesha muda wa kustaafu kwa  Wahadhiri waandamizi, Maprofesa na Madaktari Bingwa kuwa miaka 60 kwa hiari na lazima miaka 65.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya January 31


chrispiny kalinga

Serikali Yasisitiza Uwazi Shughuli Za Madini


Kampuni za Madini nchini zimetakiwa kufanya shughuli zake kwa uwazi sambamba na kufuata Sheria za nchi ili kuepuka migongano.

Wachimbaji Wanne wafariki kwa kufukiwa na kifusi Arusha


 Wachimbaji wanne wamefariki na  mmoja yupo mahututi baada ya kuangukiwa na Ngema  walipokuwa wakipakiza  changarawe kwenye gari katika machimbo ya changarawe yaliyopo katika mlima Murieti katika jiji la Arusha.

Rais Magufuli Kuzindua Pasipoti ya Kielektroniki


Na Jonas Kamaleki
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli leo  atazindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Familia ya lissu Yahofia Tundu Lissu Kufukuzwa Hospitali



Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), imelitaka Bunge kutoa fedha za matibabu yake kama halitaki mtunga sheria wake huyo akafukuzwe hospitalini alikolazwa.

Raila Odinga hatarini kushtakiwa kwa kujipa urais nchini kenya


MAMLAKA za Kenya, jana zilizima vituo vya televisheni kuzuia matangazo 'live' ya sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, ambaye alisusia uchaguzi wa marudio wa mwaka jana uliobishaniwa.

NECTA Watangaza Matokeo ya Kidato Cha Nne 2017....Bofya Hapa Kuyatazama



Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba.

LUDEWA MKUU WA WILAYA YA LUDEWA MKOANI NJOMBE ATOA KAULI NZITO JUU YA YEYOTE ATAKAYE KUTWA AMESIMAMA NA WANAFUNZI.





 Na chrispiny kalinga.

wananchi wilayani ludewa mkoani njombe katika kata ya mlingali na wanaulalamikia uongozi wa shule za sekondari zilizopo katika kata hizo kwa madai ya kutozwa chakula cha watoto wao kisicho pungua debe kumi ambazo ni sawa na kilo mia moja.

LUDEWA WALIMU WA SHULE YA MSINGI WAWAAMURU WANAFUNZI KWENDA KULIMA SHAMBA LA MWALIMU MUDA WA MASOMO.



 
Na chrispin kalinga. 
 
Walimu wilayani ludewa mkoani njombe katika kata ya lubonde shule ya msingi masimbwe wawaamrisha wanafunzi kwenda kulima shamba la mwalimu wa awali muda wa masoma.

Dinsdag, Januarie 30, 2018

SIKU 14 ZA DANGOTE VIONGOZI WAKAZA KAMBA KUMTAZAMA



Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa siku 14 kwa uongozi wa kiwanda cha saruji cha Dangonte mkoa wa Mtwara kuingia mkataba na wachimbaji wadogo wa gypsum.
Biteko ametoa kauli hiyo leo Januari 21, 2018 baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza na viongozi wake.


MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKAGUA STENDI MPYA NA SOKO NJOMBE,


Mkuu wa Mkoa Wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Akitoa maagizo Kwa wataalamu wa Ujenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Akiwa Katika Stendi mpya Njombe Mjini. 
Kulia ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Bw,Erasto Ngole Akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Katika Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Stendi mpya ya Magari Njombe mjini. 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Akitembelea na Kukagua maeneo mbalimbali Ndani ya Stendi Mpya ya Njombe, Mjimwema. 

Wakwanza Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri Aliyeambatana  na Mkuu wa Mkoa wa Njombe katika Ziara hiyo. 
Nimwonekano wa baadhi ya Maeneo katika Stendi mpya ya Magari Njombe Mjini katika eneo la Mjimwema, 
Jengo la Vyoo na Bafu Katika Stendi Mpya ya Magari Njombe Mjini.

Na Maiko Luoga Njombe,
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Mapema Leo January 23 ,2018 Ametembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi Njombe Mjini Mradi ambao unaendelea kwakusuasua na Mkandarasi hayupo Saiti.

Baada ya kukagua Stendi hiyo ya mabasi Njombe, Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe amebaini Kuwa kuta za Stendi hiyo zimejengwa Chini ya kiwango kwakuwa kabla ya Kuanza kutumika tayari Kuta hizo zimeshatengeneza Nyufa Licha ya Jengo hilo la stendi kutumia pesa nyingi za Serikali hatahivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe amewaagiza Wataalamu wa Ujenzi Kuhakikisha Sehemu zote zenye matatizo zinarekebishwa na Hatua stahiki zakisheria Zinachukuliwa Kwa wote waliosababisha Upungufu huo wa jengo la Stendi mpya ya mabasi Njombe Mjini.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Wa Njombe pia Kwakuambatana na Uongozi wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe akiwemo Katibu wa chama hicho Mkoa wa Njombe Bw. Hosea Mpagike na Katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Bw. Erasto Ngole kwapamoja wametembelea na kukagua Ujenzi wa Mradi wa Soko Jipya la Wafanyabiashara Mjini Njombe Kisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe alitoa maagizo Kwa Mkurugenzi wa mji wa Njombe Kuhakikisha ujenzi huo unakamilika Kwa haraka ili wafanyabiashara waweze kuendelea na Biashara zao.

Alipowasili Katika eneo la Soko kuu la wafanyabiashara Njombe mjini Mkuu wa Mkoa Hakuwakuta viongozi wa kata ya Njombe mjini na kupewa Maelezo kuwa viongozi hao wapo Katika kikao cha Kata ambapo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Alitoa Amri kuwa Viongozi hao waache kikao chao maramoja na kisha wahudhurie mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe akizungumza na wafanyabiashara Katika soko kuu la wafanyabiashara Njombe Mjini.
Endelea kutembelea www.maikoluoga.blogspot.com Kwa Habari zaidi
chrispiny kalinga