Woensdag, April 11, 2018

Thea Atoa Pongezi Zake kwa Makonda ....... Ni Baada ya Kampeni ya Kusaidia Wanawake

Msanii wa bongo movies Ndumbagwe Misayo maarufu kama Theaameandika ujumbe mrefu kwa ajili ya kumpongeza Mh Paul Makonda baada ya kuanzisha kampeni ya kusaidia wanawake ambao wametelekezwa na wanaume zao na kuwaachia watoto kulea peke yao.

Dinsdag, April 10, 2018

Mwanafunzi kidato cha kwanza abaka na kuua


NA MELLANIA JULIUS


Mwanafunzi wa kiume mwenye umri wa miaka 15 ambaye alikuwa anasoma kidato cha kwanza shule ya sekondari Gituto katika kaunti ya Murang'a nchini Kenya, ameuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kubainika kumbaka binti mwenye umri wa miaka 12 na kisha kumnyonga.

Dada wa binti aliyeuawa Grace Kabura, amesema alimuacha mdogo wake nyumbani, na aliporudi hakumkuta.

“Nilirudi nyumbani sikumkuta Wambui, nikawauliza watoto waliokuwa wakicheza jirani wakaniambia ameondoka na Duncan Wakahiu”, amesema dada wa binti huyo aliyeuawa.

Grace ameendelea kwa kueleza kwamba baada ya hapo aliwaomba watoto wamuonyeshe nyumbani kwa kijana huyo na kuwakuta wazazi wake, kisha akawaeleza kuwa anamtafuta mdogo wake ambaye ameonekana kuelekea hapo.

Baada ya hapo wazazi wa kijana wakamuita mtoto wao na kumuuliza mahali alipo mwenzake, akawaambia amemtuma dukani na hajarudi.

Grace ameendelea kueleza kuwa wazazi wake waliingiwa na mashaka na kuamua kupekua ndani ya chumba cha kijana wao, na kukuta mwili wa Wambui ukiwa uvunguni na kijana huyo kukimbia.

Hata hivyo wananchi waliamua kumsaka kijana huyo na walipompata walimshushia kipigo na kumuua.

mubashara blog +255753121916

Baada ya ligi kusimama hatimaye yarejea

Ligi Kuu ya soka la Wanawake Tanzania hatua ya Nane bora inatarajia kuendelea Jumapili Aprili 21 kwenye viwanja tofauti baada ya kusimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars.

Hatua hiyo ya nane bora ambayo ilisimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) iliyokuwa kambini kujiandaa na mchezo wake wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake itaendelea katika mzunguko wa 5.

WAKULIMA LUDEWAWATAKIWA KUZALISHA PARACHICHI


Na Maiko Luoga Ludewa

Wakulima wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Wameshauriwa Kuzalisha Mazao ya Biashara kwa wingi yenye Fulsa za Soko la Uhakika ndani na Nje ya Mipaka ya Tanzania.

Mashindano ya kuwabeba wake yafanyika Uingereza

Mshindi wa mchuano wa kubeba mkeHaki miliki ya pichaPA
Image captionMshindi wa mchuano wa kubeba mke
Haya ni mashindano ya 11 ya mbio za kubebana nchini Uingereza.
Chris Hepworth, akiwa amembeba Tanisha Prince kutoka West Drayton, London, alikimbia na kuibuka mshindi wa mbio za umbali wa mita 380.

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 10.04.2018: Mabadiliko yanatarajiwa katika klabu za soka

Meneja wa Chelsea Antonio Konte
Image captionKazi ya Antonio Konte katika Chelsea imo mashakani na huenda akaihama klabu hiyo msimu huu
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anakabiliwa na tishio tena la kupoteza kazi na Mtaliano huyo anaweza kuondoka kwenye wadhifa huo kabla ya mwisho wa msimu huu. (Mail)

Mfumuko wa bei wapungua Tanzania

Uchumi wa nchi za Afrika ulishuka hadi asilimia 1.6 mwaka 2016Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUchumi wa nchi za Afrika ulishuka hadi asilimia 1.6 mwaka 2016
Mfumuko wa bei nchini Tanzania unaripotiwa kupungua kwa asilimia 0.2 kutoka asilimia 4.1 hadi asilimia 3.9 ,Taasisi ya taifa ya Takwimu imeeleza

Tanzania yazindua chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi

Binti akionyesha kadi yake baada ya kupokea chanjo
Image captionBinti akionyesha kadi yake baada ya kupokea chanjo
Serikali ya Tanzania imezindua kampeni ya chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi.
Zaidi ya wasichana laki 6 walio na umri kati ya miaka 9 hadi 14 watachanjwa nchini nzima.

Sakata la kufungiwa nyimbo za wasanii Laibuka Bungeni

Sakata la kufungiwa nyimbo za wasanii limeibuka bungeni na kusababisha kelele za wabunge pande zote.

Diamond Platnumz: Kwangu Huu Sio Msalaba Bali ni Alama ya Kujumlisha Yenye Siri Nzito

Msanii mkubwa  Tanzania wa Muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul  ali maalufu kama ‘Diamond Platnumz’,   amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakimsema kuwa anavaa msalaba ambao hauendani na imani yake lakini ukweli unabaki kuwa siri ya msalaba huo anaijua yeye na kwamba kwake yeye ule sio msalaba bali ni alama ya kumjumlisha ambayo kwake ina maana sana.

Mke wa 8 wa Mfalme Mswati III, Senteni Masango amejiua kwa kunywa vidonge



Mke wa nane wa Mfalme wa Swaziland, Mswati (III), Senteni Masango amefariki  akiwa chumbani kwake wikiendi iliyopita.

TRA Trilioni 11.78 Ndani ya Miezi 9


Mamlaka ya Mapato Tanzania imekusanya Tsh Tril 11.78 katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka wa fedha 2017/18 kuanzia Julai 2017 hadi Machi 2018, ikilinganishwa na Tsh. Tril 10.86 ambazo zilikusanywa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17, ambacho ni sawa na ukuaji wa 8.46%.

Jamhuri Kumleta Mpenzi wa Nondo Kutoa Ushahidi Mahakamani

Upande wa Jamhuri katika kesi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, Veronica Fredy anatarajiwa kuletwa makamani kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili mwanafunzi huyo.