Haki miliki ya pichaFOREIGN TANZANIAImage captionDkt Mahiga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel jijini Tel Aviv
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga amezindua rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na kuitaka Israel nayo iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionWanamgambo wa kiislamu wanadhibiti maeneo kadhaa nchini Somalia
Mwanamke mmoja amepigwa na mawe mpaka kifo nchini Somalia baada ya mahakama moja inayoendeshwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu, al-Shabab kumkuta na hatia ya kuolewa na wanaume wengi.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionMlipuko wa mwisho wa Ebola DR Congo ulikuwa 2017 ambapo watu 4 walifariki
Serikali ya Kenya imeimarisha doria katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta na vituo vingine vya mpakani baada ya visa vya ugonjwa wa Ebola kuripotiwa kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize amepokea makavu live kutoka kwa mwanadada anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo movie Shamsa Ford baada ya kumuorodhesha mumewe Chidi Mapenzi Kwenye orodha ya Wolper.
Hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani, ya kutangaza kwamba nchi hiyo inajiondoa kwenye mkataba wa kimataifa wa mpango wa kuizuia Iran kutengeneza silaha za nuklia, JCPOA, imepokelewa kwa hisia kinzani na wabunge wa Marekani na viongozi mbalimbali ulimwenguni kote.
Mwanasayansi aliyesafiri kutoka Australia mpaka Uswiss David Goodall, kwa ajili ya kuukatisha uhai wake kesho inatarajiwa kuwa ndiyo siku ya kuhitimisha maisha yake ya duniani baada ya madaktari kuchomeka sindano ya sumu katika mshipa.
Serikali imesema tayari nchi imeanza rasmi majaribio ya dawa kinga mpya inayozuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi (PrEP), huku ikikanusha kuwapo kwa dawa inayotibu ugonjwa huo.
Polisi upande wa Mashariki mwa India katika jimbo la Jharkhand wamearifu kuwa wamemkamata mtuhumiwa mkuu anayehusishwa na unyanyasaji wa kingono na mauaji ya binti mdogo .
Maafisa kutoka Mashariki mwa Afghanistan wanaarifu kuwa watu kumi na nne wamekufa na wengine na kadhaa walijeruhiwa katika mlipuko kwenye msikiti katika jimbo la Khost.
Watu sita wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka bahari, karibu na Kisiwa cha Mafia Tanzania,kutokana na dhoruba kali.Mbunge wa jimbo la Mafia, mkoani Pwani Mbaraka Dau amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Rais Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa serikali kuacha kutoza ushuru kwa wananchi wanaosafirisha bidhaa na mazao ambayo hayajafika uzito wa tani moja, kwakuwa bunge mwaka 2017 lilipitisha sheria ya kufuta tozo zaidi ya 87 katika sekta ya kilimo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo, ametekeleza kwa vitendo agizo alilopewa na Rais Magufuli, la kwenda kijijini Tundu, Wilayani Mikumi kushughulikia kero ya mradi wa maji kijijini hapo.